Kiongozi huyo mwenye utata alisifiwa na wafuasi
wake kama kiongozi wa ujamaa, askari
mwanasiasa ambaye aliirejesha Cuba mikononi
mwa watu.
Lakini alikabiliwa na shutuma kwa kuwazima
wapinzani wake kwa njia ya mateso na kwa kuwa
na sera ambazo ziliporomosha uchumi wa Cuba.
Fidel Alejandro Castro Ruz alizaliwa tarehe 13
Agosti 1926, nje ya ndoa ya familia ya mkulima
bwanyenye , Angel María Bautista Castro y Argiz,
ammbaye alihamia Cuba kutoka Uhispania.
Mama yake , Lina Ruz González alikuwa kijakazi
aliyefanya shughuli za shamba ambaye baadae
alikuwa mpenzi wa baba yake ,na baadae ,baada ya
kuzaliwa kwa Fidel, akawa mkewe.
Castro alisoma katika shule ya kikatoliki mjini
Santiago kabla ya kujiunga na chuo
kinachoendeshwa na makasisi wa Jesuit- kilicho El
Colegio de Belen jijini Havana.
Hata hivyo, alishindwa kimasomo , na badala yake
alipendelea kutumia muda wake mwingi katika
shughuli za michezo.
Ilikuwa wakati anasomea sheria katika Chuo Kikuu
cha Havana kati kati ya miaka ya -1940s ndipo
alipokuwa mwanaharakati wa siasa, na kuimarisha
ujuzi wake wa kuzungumza hadharani.
Malengo yake yalikuwa ni pamoja serikali ya Cuba,
iliyoongozwa na Ramon Grau, ambayo ilikumbwa na
shutuma za ufisadi wakati huo.
Ghasia za maandamano ya upinzani ziligeuka kuwa
maisha ya kila siku na Castro akajipata akilengwa
na polisi.
Pia alikuwa miongoni mwa watu waliopanga njama
za mapinduzi ya kumg'oa mamlakani Rafael Trujillo,
kiongozi wa mrengo wa kulia wa Dominican
Republic , lakini jaribio hilo lilishindwa baada ya na
Marekani kuingilia kati.
Mnamo mwaka 1948 Castro alimuoa Mirta Diaz-
Balart, mwanae mwanasiasa tajiri nchini Cuba.
Mbali na kumtia msukumo wa kujiunga na wasomi
wa nchi, aligeuka kuwa na itikadi za he Kimaxist
Aliamini matatizo ya Cuba ya kiuchumi yalikuwa ni
matokeo ya ubepari usioweza kudhibitiwa ambao
unaweza kutatuliwa tu kwa mapinduzi.
Baada ya kuhitimu masomo Castro alizindua
shughuli za kisheria lakini zilishindwa kufanikiwa na
aliendelea kuingia katika mzozo wa madeni.
Alisalia kuwa mwanaharakati wa kisiasa, akishiriki
katika misururu ya maandamano ya mara kwa
mara ya ghasia.
Mnamo mwaka 1952 Fulgencio Batista alifanya
mapinduzi ya kijeshi yaliyomg'oa madarakani rais
wa Cuba , Carlos Prío.
Sera ya Batista ya uhusiano wa karibu na Marekani
na kukandamiza mashirika ya kijamaa vilikuwa
pingamizi kwa kwa imani za kimsingi za siasa za
Castro.
Baada ya kushindwa kisheria, Castro alibuni shirika
lililoitwa The Movement, lililoendesha shughuli zake
kisiri kwa lengo la kuung'oa madarakani utawala wa
Batista.
Cuba palikuwa mahala pa watu matajiri kujivinjari,
na nchi iliongozwa na kiasi kikubwa na magenge ya
wahalifu . Ukahaba ,wacheza kamali na walanguzi
wa mihadarati vilikithiri.
Mwezi Julai 1953 Castro alipanga shambulio dhidi
ya kituo cha kijeshi cha Moncada akaribu na
Santiago ili kupora silahga kwa ajili ya kuzitumia
katika harakati za kivita.
Shambulio lilishindwa na wanamageuzi waliuawa
ama kukamatwa . Castro alikuwa mmoja wa
wafungwa kadhaa waliofikishwa mahakamani
mnamo mwezi Septemba 1953.
Castro alitumia muonekano wake mahakamani
kutangaza maasi yaliyotekelezwa na jeshi jambo
ambalo baadae lilimpatia umaarufu, hususan
miongoni mwa waandishi wa habari wa kigeni
ambao waliruhusiwa kuhudhuria kesi hiyo.
Guerrilla warfare
Alihukumia kifungo cha miaka 15 jela . Baadae
aliachiliwa hru kufuatia tangazo la huruma la jumla
mnamo mwezi Mei 1955 baada ya kutumikia
kifungo hicho kwa miezi 19 pekeekatika mazingira
bora kiasi.
Katika kipindi hiki kifupi gerezani alimtaliki mkewe
na kujiimarisha zaidi katika sera za kimaxist.
Kutokana na Batista kuendela kuwakamata
wapinzani wake , Castro alitorokea Mexico kuepuka
kutuwa nguvuni . Huko alikutana na mwana
mageuzi kijana aliyeitwa Ernesto "Che" Guevara.
Mnamo mwezi Novemba 1956, Castro alirejea Cuba
akiambatana na wanajeshi 81 akwenye ndege
iliyokuwa na uwezo wa kuwabeba watu 12 pekee.
Makao makuu ya chama yalitafuta hifadhi katika
milima ya Sierra Maestra . Kutoka kwenye ngome
hii Castro alizingua vita vya msituni dhidi ya
utawala wa Havana.
Tarehe 2 Januari, 1959, jeshi la waasi likaingia
katika mji mkuu wa Cubanna Batista akatoroka.
Mamia ya wafuasi wa zamani wa Batista
walinyongwa baada ya kesi ambazo wageni wengi
waliziona kuwa hazikuwa za haki.
Castro ralijibu kwa kusisitiza kwamba " Haki ya
mageuzi haina misingi ya kisheria ya kubadili tabia
ama mawazo , bali inazingatia uwajibikaji wa
maadili ".
Serikali mpya ya Cuba iliahidi kurejesha ardhi kwa
watu na kulinda haki za maskini.
Lakini mara moja serikali ilianza kulazimisha
mfumo wa chama kimoja cha kisiasa . Mamia ya
watu walitupwa jela na kwenye kambi za
kutumikisha kazi za sulba kama wafungwa wa
kisiasa.
Maelfu ya waCuba hususan wenye kipato cha kadri
wakalazimika kuikimbia nchi yao.
Castro alisisitiza kwamba fikra zake zilikuwa ni
bora zinajali kwanza maslahi ya watu wa Cuba.
"hakuna ujamaa au umaxist , bali uwakilishi wa
demokrasia na haki ya kijamiikatika mpango bora
wa uchumi ," alisema wakati huo.
Mnamo 1960, Fidel Castro naliwapatia uraia
wamarekani woote waliokuwa wanamiliki biashara
katika kisiwa hicho.
Kujibu hatua hiyo, utawala wa Washington
ulimuwekea vikwazo vya kibiashara vilivyo tarajiwa
kudumu kwa karne ya 21st century.
Castro alidai kuwa alilazimishwa kuingia katika
mikono ya muungao wa Usovieti na kiongozi wake ,
Nikita Khrushchev, ingawa baadhi ya wachanganuzi
walisema aliingia katika muungano huo USSR kwa
utashi wake mwenyewe.
Iwe sababu yoyote ile, taifa la Cuba liligeuka kuwa
uwanja wa mapamabano ya vita baridi vya dunia.
Mwezi Aprili 1961, Marekani ilijaribu kuipindua
serikali ya Castro kwa kuwapatia mafunzo
wanajeshi binafsi wa Cuba waliokuwa ukimbizini ili
kuvamia kisiwa hicho.
Katika mwambao wa Pigs,vikosi vya Cuba vilikabili
majeshi ya uvamizi , na kuwauwa wengi huku 1,000
wakikamatwa. Fidel Castro alikuwa ameonja malaka
kwa njia ya damu kwa hivyo asingeweza
kuwasamehe.
Mwaka mmoja baadae, ndege za uchunguzi za
Marekani ziligundua makombora ya Usovieti wakati
zilipokuwa njiani kuelekea maeneo ya Cuba.
Dunia ilishtushwa na uwezekano wa kutokea vita
vya nuklia .
"msururu wa maeneo yenye makombora ya masafa
marefu ya kivita sasa yanaandaliwa katika kisiwa
kilichofungwa. Lengo la ngome hizi za makombora
haliwezi kuwa lingine zaidi ya kutoa uwezo wa
kufanya mashambulio ya nuklia dhidi ya mataifa ya
magharibi ," alionya rais John F Kennedy.
Mataifa yenye nguvu duniani yalibaki kushuhudia
kinachoendelea lakini ni rais Khrushchev pekee
ambaye aliweza kuchukua hatua kwanza na
kuondoa makombora yake nje ya Cuba baada
Marekani kukubali kuondoa kisiri silaha zake
kutoka Uturuki.
Fidel Castro, hata hivyo , alikuwa tayari ni adui wa
Marekani namba moja. Maafisa wa ujasusi wa
Marekani CIA walijaribu kumuua , katika kisa
kilichojulikana kama -Operation Mongoose ambapo
mbinu mojawapo ilikuwa apewe sigara iliyokuwa
imesheheni vilipuzi.
Mbinu nyingine zilikuwa za kushangaza , ikiwemo
mojawapo ya kumfanya ndevu zake zianguke ili
kumfanya awe na sura ya kuto heshimika.
Muungano wa Usovieti ulimwaga pesa ndani ya
Cuba. Ulinunua mavuno ya sukari inayozalishwa
kisiwani humo na meli zake kurejea na zimesheheni
na bidhaa nyingine, kama vile chakula kilichokua
kinahitajika ili kukabiliana na vikwazo vya Marekani
vya biashara.
Licha ya utegemezi wa msaada kutoka mataifa ya
Usovieti , Castro aliiongoza Cuba kuwa taifa jipya
lisilokuwa na mafungamano yoyote.
Hata hivyo, aliegamia hasa Afrika, ambako alituma
majeshi kuunga mkono wapiganaji wa msituni
waliokuwa na sera za kimaxist katika nchi za
Angola na Msumbiji.
Kati kati ya miaka ya 1980 , hata hivyo, siasa za
dunia za maeneo zilibadili mkondo wake . Ilikuwa ni
enzi ya Mikhail Gorbachev, sera za glasnost na
perestroika, na zilidhihirika wazi kuwa kinyume na
mageuzi ya Castro.
Utawala wa Moscow ukakata uhusiano wa
kiuchumi maramoja na Cuba kwa kukataa kata kata
kununua sukari ya Cuba.
Akiwa bado chini ya vikwazo vya Marekani na
kukatwa kwa huduma muhimu za mataifa ya Soviet
, uhaba wa kudumu wa bidhaa na ukosefu wa akiba
ya bidhaa vilidhihirika ndani ya Cuba
Jazba ilipanda huku misururu ya kupata ikiendelea
kurefuka.
Taifa ambalo Fidel Castro aliita lililoendelea zaidi
duniani, hali ya maisha ilikuwa mbaya.
Katika kati ya miaka ya -1990s, waCuba wengi
walikuwa wamechoshwa na hali nchini mwao.
Maelfu walianza kutoroka kupitia njia ya maji hadi
Florida wakiwa na ndoto ya kuishi maisha bora
zaidi. Wengi walikufa maji, lakini ilikuwa kura tosha
ya kutokuwa na imani na Castro.
Hata hivyo Cuba ilirekodi baadhi ya mafanikio ya
kufurahisha ndani ya nchi. Huduma bora za
matibabu zilitolewa bure kwa wote , na viwango vya
vifo vya watoto wachanga wa vililinganishwa na
vile vya mataifa tajiri duniani.
Katika miaka iliyofuata , Castro alionekana mtulivu .
Mwaka 1998 alitembelewa na Papa John Paul II,
jambo ambalo halingeweza hata kufikiriwa miaka
mitano ya awali.
Wakati huo Papa aliilaumu Cuba kwa ukiukaji wake
wa haki za binadamu , na kumuaibisha Castro
mbele ya vyombo vya habari vya dunia.
Fidel Castro alikuwa amebuni utambulisho wake
kama mjamaa wa Caribbean ambao kwa miaka
kumi iliyopita , alilazimika kuukumbatia , pole pole
alianzisha mabadiliko machache ya biashara huria
ili kulinda mageuzi yake.
Tarehe 31 Julai 2006,siku chache tu kabla ya
maadhimisho ya mwaka wake wa 80 wa kuzaliwa,
Castro alikabidhi mamlaka ya muda kwa Raul baada
ya kufanyiwa upasuaji wa dharura wa utumbo.
Afya yake iliendelea kudhoofika. Mapema mwaka
2008, Castro alitangaza kwamba hatakubali nyadfa
za urais na amiri jeshi mkuu katika mkutano kuu
ujao wa kitaifa.
Katika barua iliyochapishwa katika gazeti rasmi la
kijamaa, alikaririwa akisema kuwa : " Ni
kudanganya nafsi yangu kuchukua majukumu
yanayohitaji kutembea na kujitolea , wakati siko
katika hali ya kimwili inayoniruhusu kufanya hivyo ."
Alijiondoa kwa kiasi kikubwa katika maisha ya
umma , huku akiandika taarifa zilizochapishwa
katika vyombo vya habari vya kitaifachini ya
kichwa cha habari...Tathmini ya maisha ya amir
Fidel.
Alijitokeza tena mwezi Julai 2010, alipoonekana
mbele ya umma tangu augue, akiwasalimia
wafanyakazi na kuhojiwa na televisheni ambapo
alijadili kuhusu hali ya wasi wasi baina ya Marekani
na Iran pamoja na Korea kaskazini.
Mwezi uliofuatia Castro alitoa hotuba yake ya
kwanza katika bunge la taifa baada ya miaka minne,
akiitaka Marekani kuacha kuchukua hatua za
kijeshi dhidi ya Iran au Korea Kaskazini akionya
kutokea kwa maafa ya nuklia ikiwa uhasama
utazidi.
Alipoulizwa a ikiwa Castro anaweza kuingia tena
katika serikali , waziri wa utamaduni Abel Prieto
aliiambia BBC: "nadhani wakati wote amekuwa
katika maisha ya siasa za Cuba lakini hayuko
serikalini. Wakati wote amekuwa makini kwa hilo.
Vita vyake vikuu ni kuhusu masuala ya kimataifa."
Tangazo la rais Obama la Disemba 2014 la
mwanzo wa kumalizika kwa vikwazo vya Marekani
vya biashara na vinginevyo lilionekana kama
matumaini katika kile kilichokuwa uadui wa nusu
karne uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Castro aliafiki hatua hiyo aliyoielezea kuwa " hatua
nzuri ya kutafuta mani ya kikanda ", lakini
hakuiamini serikali ya Marekani.
Wakati waCuba wengi bila shaka hawakumpenda
Castro, wengine walimpenda kwa dhati . Walimuona
kama David ambaye aliweza kukabiliana na Goliath
wa Marekani.
Kwao Castro alikuwa Cuba na Cuba ilikuwa Castro.
Tags
MAKALA