Nahodha wa klabu ya Man United Wayne Rooney wiki hii iliripotiwa na vyombo vingi vya habari kuwa klabu ya inayoshiriki ligi kuu ya chini Shanghai Shenhua kuomba kumsajili kutoka klabu yake ya Man United na kwenda kuanza maisha mapya ya soka nje ya uingereza kwa mara ya kwanza
Klabu ya Shanghai Shenhua ilianza kuiomba Man United kumsajili Wayne Rooney kwa dau la pound milioni 27 mwishoni mwa mwaka 2015, kwa sasa inamuhitaji na ilitaka kumlipa mshahara wa pound 500,000 kwa wiki,kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mshahara huo ni mara mbili ya anaolipwa kwa sasa na Man United, kitu ambacho kingemfanya Wayne Rooney avune zaidi ya Tsh bilioni 200 za kitanzania kwa kipindi cha miaka mitatu.
Fedha hizo ni nje ya posho na bonasi za mechi.
Licha ya dili hili kuwa zuri sana kwa Wayne Rooney lakini gazeti Sunday Times limeripoti kuwa mshambuliaji huyo wa uingereza ameitolea nje ofa hiyo ya wachina.
Klabu hiyo ya China yenye jeuri ya fedha ilishawahi kuwasajili Didier Drogba na Nicolas Anelka inaonekana imegonga mwamba katika mpango wao wa kumfanya Rooney ajiunge nao licha ya ofa nono waliyotoa.