TP Mazembe wamechukua kombe la "Caf super cup" kwa kuifunga timu ya Etoile du Sahel kwa magoli 2-1.
Mchezaji wa TP Mazembe D.Adjei Nii ndie aliefunga magoli yote mawili huku goli la kufutia machozi kwa upande wa Etoile du Sahel likifungwa na Iheb Msakni.
Kwa kuchukua kombe hilo la Super cup Inawafanya TP Mazembe kuwa mabingwa mara tatu wa super cup kwani walifanya hivyo mwaka 2010 na 2011.
Super Cup ni kombe linalowakutanisha bingwa wa klabu bingwa africa dhidi ya bingwa wa kombe la shirikisho.
Tags
Michezo