Kipa wa Manchester City Willy Cabalero aliibuka shujaa wa mechi ya fainali ya Capital One Cup kati ya Man City na Liverpool baaya ya kucheza penati tatu za Liverpool na kuisaidia timu yake kuchukua ubingwa huo.
Timu hizo zilizotoshana nguvu katika dakika 90 za kawaida na zile 30 za nyongeza baada ya kumalia kwa goli1-1.
Man City ndio walioanza kupata goli kupitia kiungo wao Fernandinho katika dakika ya 49 kabla ya Liverpool kusawazisha kupitia kwa Coutinho dakika ya 83.
Hadi dakika 90 zinaisha matokeo yalisomeka 1-1 ndipo ukaongezwa muda wa ziada wa dakika 30.
Dakika hizo hazikuweza kuzaa goli kwa upande wowote ndipo uamuzi wa penati ukafuatia ili kuamua nani aondoke na kombe hilo.
Liverpool walianza kwa kupati penati ya kwanza kisha man City wakakosa.
Mambo yakabadilika ghafla kwani Liverpool walikosa penati tatu zote zilizofuatia baada ya wachezaji wao kupiga penati ambazo kipa wa City aliziona na kuzicheza kwa ufundi wa hali ya juu.
Kiungo wa City anayetokea Ivory Coast aliwanyanyua mashabiki wa Man City baada ya kufunga penati ya mwisho iliyowapa ubingwa kwa ushindi wa penati 3-1.