Mchezaji kinda wa Manchester united, Rashford mwenye umri wa miaka 18 tu jana aliibuka shujaa wa mechi ya wapinzani wa EPL Manchester United dhidi ya Arsenal baada ya kufunga magoli mawili ya haraka yalioisaidia Man U kuibuka wababe.
Rashford ambae ni mechi yake ya pili kuichezea Man U aliandika goli la kwanza katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza.
Ilimchukua dakika tatu tu kuongeza goli la pili alilofunga kwa kichwa mnamo dakika ya 32 ya mchezo huo.
Lakini katika dakika ya 40 mchezaji wa zamani wa Man U Danny Welbeck aliifunga timu yake ya zamani na kufanya matokeo kusomeka 2-1 hadi half time.
Andy herrera alipachika goli la tatu baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Rashford na kuipa Man U uongozi wa goli 3-1.
Dakika nne baadae Arsenal waliamka na kupata goli dakika ya 69 kupitia kwa Kiungo Mesut Ozil.
Hadi dakika 90 zinamalizika Man U waliondoka na point tatu muhimu dhidi ya Arsenal ambayo imeanza kupoteza uelekeo wa kupata ubingwa wa Epl huku kinda wa Man U Rashford akiibuka shujaa baada ya kuidungua Arsenal goli mbili na kutengeneza moja.