Mchezaji wa kitanzania anayechezea klabu ya Genk inayoshiriki ligi kuu ya Belgium,Mbwana Samata jana usiku aliweza kuondoa 'gundu' na kufunga goli lake la kwanza katika klabu hiyo.
Genk iliokua ikimenyana na club brugge katika mchezo wa ligi kuu nchini humo na alikuwa ni samata aliefunga goli lililowahakikishia ushindi Genk.
Brugge ndio walianza kupata goli katika dakika ya 15 kipindi cha kwanza kupitia kwa Meunier kisha Genk wakaja kusawazisha dakika ya 36 kwa njia ya penati iliopigwa na Karelis na hivyo kufanya matokeo kusomeka 1-1 hadi half time.
Kipindi cha pili Genk waliongeza goli la pili lililofungwa na Buffel katika dakika ya 50.
Mtanzania Mbwana Samata alieingia kutokea benchi alipigilia msumari wa tatu katika dakika ya 81 na kuihakikishia Genk ushindi.
Brugge walipatia goli la pili dakika mbili tu baadae lakini hilo haliwakusaidia kuepuka kichapo.
Goli hilo ni la kwanza kabisa kwa Mbwana Samata katika maisha yake ya Soka ulaya.
Swahiba Media inamtakia kila la kheri mtanzania huyo anaeiwakilisha nchi yetu katika ligi hiyo.