VIDEO Queen asiyeishiwa na matukio, Anna Kimario ‘Tunda’ ameibuka na kudai kuwa anaolewa hivi karibuni na mwanaume ambaye sio staa kwani ameshavalishwa pete ya uchumba. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Tunda alisema pete ambayo inaonekana kidoleni mwake siyo feki kama baadhi ya watu wanavyodhani na watu wajue kwamba ‘anayebeba mzigo jumla’ ni mwanaume wa kawaida na siyo staa.
“Naolewa soon, tena nafurahi kuwa naolewa na mtu ninayempenda na anayejielewa na sio kama drama za wale watu wengine waliopita, nimeamua kujituliza tofauti na unavyonijua huko nilipotoka,” alisema Tunda