Meya wa Pennsylvania, Sharif Street na Meya wa Philadelphia, Jim Kenney wametangaza kuwa kuanzia Machi 14 hadi 17 ni itakuwa ni wikiendi ya Meek Mill “Meek Mill Weekend” ambapo wakazi wa jimbo hilo watatafakari kazi za Meek Mill na kujifunza kupitia nyimbo zake kwenye maeneo ya starehe na majumbani.
Kwenye tamko lililotolewa Alhamisi ya wiki hii katika ukumbi wa City Hall mjini humo, Meek Mill alikuwepo na alikabidhiwa Cheti cha kutambua mchango wake kwenye jimbo hilo ambalo ndiko alikozaliwa.
“Tunajua jimbo letu lilivyokuwa zamani na ukilinganisha na sasa hivi. Bila shaka kazi za Meek Mill zimesaidia vijana wengi kuachana na vitendo vya kihalifu, na kama serikali tumeamua kuanzia Machi 14-17 itakuwa siku maalumu kwake ya watu kutafakari kazi zake,“amesema Shareef.
Mwaka jana mwezi April Meek Mill aliachiwa kwa dhamana baada ya kukaa jela kwa miezi mitano