kiwanja hakiuzwiiii

 

Ogopa Matapeli Wasije Wakakuuzia Mpanzu wa Bei ya Jioni….

Kituo kimoja cha Radio kimeripoti kuwa Mpanzu ameomba kuondoka Simba kwa kuwa amepata timu na anataka kununua Mkataba wake ambao thamani ya kuvunja Mkataba huo ni Milion 350

Taarifa hii ni mwendelezo wa taarifa za makusudi zenye lengo la kuzua taharuki ndani ya klabu yetu

Hakuna ofa yeyote ya Elia Mpanzu iliyowasilishwa kwenye klabu yetu wala mchezaji mwenyewe hajawasilisha ombi la aina hiyo

Kama haitoshi gharama ya kununua Mkataba wa Mpanzu ni zaidi ya thamani iliyotajwa na Radio hiyo

Kwa ufupi ni kwamba Volcano ataendelea kusalia Unyamani kwa misimu mingine ijayo

Kwenye mpango wa kuboresha kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao jukumu letu ni kuwabakisha Wachezaji wetu bora kisha kuongeza bora wengine

Post a Comment

Previous Post Next Post