DAWA YA ASILI YA KUZUIA MIMBA KUHARIBIKA

Admin
By -
0
Mimba kuharibika ni tukio linalowatokea wanawake na mamalia wengine wa kike kutokana na shida mbalimbali katika ukuaji wa mimba tumboni mwa mama.

Ni tukio tofauti na utoaji mimba ambalo linasababishwa na binadamu kwa makusudi.

Matukio yote mawili kwa kawaida yanaleta matatizo mbalimbali kwa mama.
Kuharibika kwa kijusi au kiinitete pengine kunatokana na mfadhaiko wa kiajali au sababu za kimaumbile.

Mimba nyingi huharibika kutokana na kutonakiliwa kisahihi kwa kromosomu; pia huweza kuharibika kutokana na mazingira.

Mimba inayotamatika kabla ya wiki ya 37 katika kipindi cha ujauzito husababisha uzaaji wa mtoto hai na hujulikana kama kuzaliwa mapema au njiti.

Kijusi akifa akiwa ndani ya chupa ya uzazi baada ya wiki ya 22, au wakati wa kujifungua, kwa kawaida hujulikana kama mzaliwa-mfu au si-riziki.

Kuzaa mapema na uzazimfu kwa jumla hauchukuliwi kama kuharibika mimba ingawa matumizi ya maneno haya wakati mwingine huingiliana.

Kati ya asilimia 10 na 50 ya mimba hutamatishwa kwa njia zinazoweza kubainishwa kimatibabu, kutegemea umri na afya ya mwanamke mjamzito.

Mimba nyingi huharibika katika hatua za mapema sana za ujauzito, kiasi kwamba mwanamke hafahamu kwamba alikuwa mjamzito.

Utafiti mmoja uliofanywa kupima homoni za kutoa yai na ujauzito uligundua kuwa asilimia 61.9 ya uhamili ulipotezwa kabla ya wiki ya 12, na asilimia 91.7 ya kuhabirika huko kulitokea bila kuonyesha dalili kabla, na bila ya fahamu ya mwanamke aliyekuwa mjamzito.

Hatari ya kutoka mimba ghafla hupungua kwa kiasi kikubwa baada ya wiki 10 kutoka kipindi cha mwisho cha hedhi.

Nini husababisha mimba kuharibika?

Kisababishi kikuu cha mimba kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza huwa ni pamoja na;

*Matatizo ya kromosomu ya kiinitete / kijusi, hali ambayo husababisha angalau asilimia 50 ya kutoka kwa mimba mapema.
*Magonjwa ya mishipa (lupus),
*Kisukari
*Matatizo ya kihomoni
*Maambukizi kama vile U.T.I 
*Matatizo ya chupa ya uzazi.
*Magonjwa ya figo
*Miali (radiation)
*Magonjwa ya moyo
*Baadhi ya dawa za kutibu magonjwa kama vile dawa ya kutibu chunusi iitwayo ‘accutane’
*Lishe duni sana
*Uvutaji sigara au tumbaku
*Utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe
*Inaweza pia kusababishwa na kiwewe kinachotokana na ajali.

Pia umri mkubwa wa mama na historia ya mimba zilizotangulia kuharibika ni sababu mbili kuu zinazohusishwa kwa sana na mimba kuharibika ghafla.

Tafiti zinazoonyesha hatari ya mimba kuharibika huwa ni asilia 12 hadi 15 katika umri wa miaka 20 na kuongezeka hadi asilimia 25 kuanzia umri wa miaka 40.

Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba mfadhaiko yaani stress au tendo la ndoa vinaweza kupelekea kuharibika kwa ujauzito.

Wakati mwingine ikiwa mama atapata matibabu kwa magonjwa sugu yanayomsumbua kunaongeza uwezekano mkubwa wa ujauzito kutokuharibika.

Dalili za mimba kuharibika

*Kuvuja damu
*Mikakamao ya mishipa
*Maumivu yasiyo ya kawaida
*Homa

Ikiwa wewe ni mjamzito na unatokewa na dalili hizo hapo juu unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka.

Dawa ya Asili ya kuzuia mimba kutoka > Unga wa Mizizi ya Maca

Unga wa mizizi ya Maca

Maca ni dawa ama chakula kinachoimarisha afya ya mfumo mzima wa homoni huku ikizisaidia kuwa na afya bora tezi za pituitari, adreno na thyroid (hizi zote ni tezi zinazohusika na kazi za kuweka sawa homoni).

Maca inao uwezo wa kuzidhibiti homoni mhimu kwa wote mwanamke na mwanaume bila yenyewe Maca kuwa na homoni nyingine ndani yake.

Maca husaidia kuisisimua au kuiamsha tezi ya pituitari. Wakati tezi hii inapokuwa imewezeshwa kufanya kazi zake kwa usahihi na kwa kiwango kinachohitajika, mfumo mzima wa homoni unakuwa sawa.

Katika mwili wa mwanamke Maca inafanya kazi ya kuidhibiti na kuiweka sawa homoni mhimu ijulikanayo kama ‘estrogen’.

Usawa wa homoni hii ya Estrogen ukiwa juu zaidi au chini zaidi ya inavyohitajika unaweza kupelekea mwanamke kutopata ujauzito au ujauzito wake kuharibika kirahisi mwezi mmoja mpaka mitatu ya mwanzo.

Usawa uliozidi wa homoni hii ya estrogen unaweza kupelekea usawa wa homoni nyingine inayohusika na uzazi ‘progesterone’ kuwa wa chini sana.

Maca inasaidia kuongeza kiwango cha homoni ya progesterone jambo ambalo ni mhimu ili kubaki na ujauzito wenye afya na salama.

Mara zote kinga ni bora kuliko tiba.

Dawa hii inashauriwa itumike mwezi mmoja kabla na miezi miwili baada ya kuwa na ujauzito ili kukupa ujauzito usio na mgogoro na kuzuia mimba kuharibika kirahisi.

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)