Kamati ya kimataifa ya michuano ya Olimpiki, imeifungia Urusi kushiriki michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itayofanyika katika jiji la Pyeongchang nchini Korea kusini mwakani.

Maamuzi hayo yamefikiwa jana na Rais wa IOC, Thomas Bach na bodi yake huko nchini Switzerland, baada ya uchunguzi wa miezi kumi na saba juu ya tuhuma za wachezaji wa Urusi kujihusisha na udanganyifu wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
Mbali na kosa hilo pia IOC iliituhumu Serikali ya Urusi kuhusika katika udanganyifu wa kuanda michuano ya olimpiki iliyofanyika nchini humo mwaka 2014 .
Uchunguzi huo ulikuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa IOC, Samuel Schmid, Licha adhabu hiyo wanariadha wa Urusi wanaweza shiriki michuano ya majira ya baridi kama wanariadha huru .
Post a Comment
0Comments
3/related/default