MWANDISHI WA HABARI AFARIKI DUNIA

Admin
By -
0


Dar es Salaam. Mwandishi mwandamizi, Joyce Mmasi amefariki dunia jijini Dar es Salaam.

Joyce amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 6,2017 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Andrew Kamugisha ambaye ni mume wa Joyce amesema mkewe alifariki saa kumi usiku katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Amesema Joyce aligundulika kuwa na saratani ya damu. Kutokana na tatizo hilo, utengenezaji wadamu ikiwemo rojorojo lililoko katika mifupa (bone marrow) na hivyo kusababisha mfumo wa chembe hai kutofanya kazi inavyotakiwa.

Kamugisha amesema hali hiyo ilisababisha Joyce aongezewe damu mara kadhaa.

Amesema wanaendelea na mipango ya maziko nyumbani kwao Mbezi Kibanda cha Mkaa jijini Dar es Salaam.

Joyce alizaliwa Juni 18, 1978 mkoani Kilimanjaro. Alisoma Shule ya Msingi Mbokomu na sekondari ya Kimbo kabla ya kujiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro.

Baada ya masomo alijiunga na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) mwaka 2000 kabla ya kwenda nchini Uganda kwa masomo ya Shahada ya Kwanza ya uandishi wa habari katika Chuo cha Uganda International.

Aliporejea nchini aliendelea kufanya kazi MCL akiwa mwandishi mwandamizi wa habari za siasa kabla ya kuamua kuacha Machi, 2017 na kujikita katika ujasiriamali na masomo ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Dar es Salaam.



Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)