Klabu ya Barcelona imegoma kutoa heshima maalum kwa Real Madrid kuelekea mc hezo wao wa Jumamosi hii mara baada ya Madrid kufanikiwa kutwa aubingwa wa Klabu Bingwa Dunia.
Kikosi cha Real Madrid kinachonolewa na Zinedine Zidane kilitwaa ubingwa huo juzi kwa kuifunga Gremio ya Brazil bao 1-0, ambapo baada ya mechi hiyo, staa wa Madrid, Cristiano Ronaldo alisema anashauri Barcelona wawape heshima kabla ya timu hizo mbili kukutana.
Kitendo hicho huwa kinafanywa na timu iliyotwaa ubingwa katika michuano husika, hivyo wapinzani wanawapa heshima kabla ya mchezo hasa kama ligi hiyo ikiwa haijamalizika.
Mkurugenzi wa Barcelona, Nou Camp, Guillermo Amor amesema hakuna kitu kama hicho na hakiwezo kufanyika kwa kuwa Madrid imetwaa ubingwa wa michuano mingine wakati wao wanakutana katika La Liga.
Post a Comment
0Comments
3/related/default