ZIJUE DALILI ZA TEZI DUME

Admin
By -
0

DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME

Uonapo dalili zifuatazo unaweza kuanza kuhisi una saratani ya tezi dume:

Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usikuKushindwa kuzuia mkojo, yaani ukichelewa kidogo unaweza kukutoka bila brekiMaumivu wakati unakojoaKuishiwa nguvu za kiumeKupungua kwa uwingi wa mbegu (low sperm count)Maumivu wakati unafika kileleniDamu kutokea kwenye mkojo au kwenye mbegu za kiumeMaumivu nyuma ya mgongo au hata nyonga nk

Uonapo dalili hizi muone daktari kwa vipimo zaidi. Kumbuka dalili tu haitoshi kukuambia una saratani ya tezi dume kwani dalili nyingine zinaweza kuwa ni dalili za ugonjwa mwingine ambao hata hauhusiani na tezi dume.



Madini ya saliniamu ni dawa ya Saratani ya tezi dume ulikuwa huifahamu bado

Hii ni ripoti mhimu kuliko zote umewahi kusoma kuhusu Saratani ya tezi dume mpaka sasa. Nitakuonyesha ni kwanini madini haya yanachukuliwa kama ndiyo dawa bora zaidi katika kuzuia na kutibu Saratani ya tezi dume (Prostate Cancer) ugonjwa ambao unaongoza kwa kuua wanaume duniani kwa sasa.

Madini ya saliniamu ni dawa ya Saratani ya tezi dume ulikuwa huifahamu bado

Kuna uhusiano wa moja kwa moja wa kiasi cha madini ya Saliniamu (selenium) ulichonacho mwilini mwako na ugonjwa wa kansa. Labda unaweza kupima kwanza kuona kama una kiasi cha kutosha cha madini haya kwenye mwili wako na ikiwa yapo chini ya kiwango kuna uwezekano mkubwa kuwa ndiyo sababu ya wewe kuugua huo ugonjwa wa tezi dume.

Dozi yake pia ni rahisi, unahitaji kutumia kiasi cha 200 micrograms cha madini haya kwa siku na utaweza kupunguza uwepo wa ugonjwa huu kwa zaidi ya asilimia 63.

Asilimia 63 siyo jambo la kitoto si ndiyo?

Sasa yanafanyaje kazi haya madini?

Kwahiyo utakuwa unataka kuniuliza yanafanyajefanyaje sasa haya madini ili kuzuia na hata kutibu saratani ya tezi dume?

Sikia. Madini haya yanayo uwezo wa kuzizuia seli za kansa kuzaliwa na kujizidisha mwanzoni kabisa mwa kuundwa kwake. Kwahiyo kansa inazuiliwa tangu mwanzoni inapotaka kutokea na madini haya ya saliniamu.

Utakubaliana na mimi sasa kwamba hii ni ripoti mhimu zaidi kuhusu saratani ya tezi dume umewahi kuisoma kwamba madini ya saliniamu yanaweza kuizuia saratani ya tezi dume kutokea kwakuwa ugonjwa huu ndiyo ugonjwa unaoongoza kuua maelfu ya wanaume kwa sasa.

Kabla hujaondoka, subiri kidogo. Siyo kwamba madini haya yanazuia tu seli za saratani ya tezi dume kutokea …. Bali pia ni dawa bora kabisa kwa kutibu ugonjwa huu.

Endelea kusoma …



Tafiti nyingi zimeendelea kuthibitisha kwamba madini ya saliniamu yanaweza kusaidia kupunguza kuongezeka kwa saratani na hata kuitibu kabisa ikiwemo saratani ya tezi dume kwa watu ambao tayari wanaugua ugonjwa huu.

Na watafiti wamegundua kuwa nguvu ya madini ya saliniamu inakuwa kubwa zaidi ikitumika sambamba na vitamini C, vitamini E na beta carotene!

Sasa hii saliniamu ubora wake inategemea na udongo ambako vyakula vyenye madini haya vinalimwa. Kwa mfano kwa sasa utaona maeneo mengi ya Ulaya na hata Amerika ardhi haina uwezo huo kama ile ya kwetu hapa Afrika na Tanzania. Kwahiyo sisi tuna uwezo mkubwa wa kupona saratani ya tezi dume kirahisi zaidi kuliko wenzetu wazungu.

Wanaume wanaotumia kiasi kingi cha madini ya saliniamu, vitamini C na E wana uwezekano mdogo sana wa kuugua ugonjwa wa saratani ya tezi dume.

Kwahiyo, mpaka sasa unapotaka kujitibu kansa ya tezi dume madini ya saliniamu yawe ni namba moja yako katika vitu unavyotumia kila siku.

Utapata wapi sasa haya madini ya saliniamu?

Namna rahisi ni kutumia dawa lishe maalumu (supplements) ambazo huandaliwa viwandani hasa kwa ajili ya watu wanaoishi katika nchi ambazo udongo wao hauna madini haya ya saliniamu kwa wingi.

Kwa wewe mwenzangu ambaye Mungu bado amekujaalia kuwa bado na ardhi nzuri madini ya salianiamu yanapatikana, ukitumia vyakula vifuatavyo kila siku ni hakika utapona ugonjwa huu na ushuhuda utaniletea.

Vyakula vyenye madini ya saliniamu kwa wingi ni pamoja na:

1. Mbegu za maboga



Sehemu kubwa ya Ulaya mbegu za maboga zinatumika kama dawa kamili ya kutibu saratani ya tezi dume. Mbegu hizi zina kiasi kingi cha madini ya saliniamu, madini ya zinki na madini mengine mhimu yaliyothibitika kudhibiti saratani ya tezi dume.

Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume.

NAMNA NZURI YA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA KAMA DAWA:

Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 5 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga, ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kila siku. Unatafuna na ganda lake hasa kama zimekaangwa tayari.

Unaweza pia kuzisaga na mashine maalumu au kuzitwanga katika kinu na utapata unga wake na utumie vijiko vikubwa viwili kutwa mara 1 kwenye kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au katika uji.

Unaweza pia kuchanganya kwenye unga wa lishe wa mtoto

Kwa muda gani? Kwa wiki 3 mpaka 4. Kumbuka pia unaweza kutumia mbegu hizi hata kama huumwi chochote!


2. Mayai ya Kienyeji



Wote tunafahamu mayai ni moja ya vyakula bora zaidi kuliko vyote chini ya jua. Mayai ni chanzo kizuri cha protini yenye thamani zaidi katika mwili wa binadamu.

Yai moja kubwa la kienyeji lina 13.9 mcg za madini ya saliniamu ambayo ni kama asilimia 20 ya kiasi cha saliniamu unachohitaji kwa siku. Mayai yana faida nyingine lukuki ndani ya mwili.

Kama una saratani ya tezi dume kula mayai mawili ya kuku wa kienyeji kila siku.

3. Uyoga



Uyoga ni moja ya vyakula vingine vyenye madini ya saliniamu. Uyoga unaweza kupikwa, kuchemshwa au kukaangwa. Kuna kama 11.9 mcg ambayo ni asilimia 17 ya saliniamu katika gramu 100 za uyoga. Uyoga ni chanzo kizuri pia cha madini ya chuma, shaba, potasiamu, riboflavin, niacin, vitamini C na vitamini D.

Uyoga pia una kiasi kingi cha nyuzinyuzi (fibre), hauna kalori nyingi wala wanga mwingi sana hivyo uyoga unaweza kutumika sambamba na mlo wowote katika siku.

Una saratani ya tezi dume? Usikose uyoga kwenye chakula chako kila siku na saliniamu utakuwa nayo ya kutosha katika mwili wako na hivyo saratani ya tezi dume utaisikia redioni.

4. Nyama ya Kuku wa Kienyeji

Mimi napenda zaidi supu ya kuku lakini kama atakaangwa au kuchomwa tu moto bado napenda kuku hata iwe ni kila siku naweza kula bila kuchoka.

Gramu 100 za nyama ya kuku wa kienyeji ina 27.6 mcg za madini ya saliniamu ambayo ni kama asilimia 39 ya mahitaji yako ya saliniamu kwa siku. Nyama ya kuku pia ni chanzo kizuri cha protini nzuri isiyo na madhara.

Pia kuna Vitamini B6 na Niacin katika nyama ya kuku. Ni chanzo kizuri pia cha madini kama ya zinki, potasiamu, riboflavin na phosphorous.

Hata hivyo nyama ya kuku kama ilivyo nyama ya kawaida ina kolesto hivyo usile kwa kuzidisha, kiasi kidogo tu tuseme robo ya kuku kwa siku inakutosha na wakati unaipika epuka kuongeza mafuta zaidi.

5. Samaki anaitwa Jodari (Tuna)

6. BataMzinga

7. Samaki anaitwa Kaa (crabs)

8. Samaki anaitwa Samoni. Ni samaki mkubwa mwenye mnofu mwekundu (Salmon)

9. Broccoli

10. Kabeji

11. Ufuta

12. Tangawizi

Ni hivyo tu, hakuna miujiza hapo.


Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)