WASANII WA WCB WAZUIWA KUTOA ALBUM

Admin
By -
0
Wakati Diamond akiwa tayari ameshatangaza ujio wa albamu yake ‘A Boy From Tandale’, imebainika katika label ya WCB kuna baadhi ya wasanii wameshindwa kutoa albamu kupisha kwanza hiyo.

Akizungumza na kipindi cha Daladala Beat, Magic Fm msanii Rich Mavoko amesema yeye pamoja na wasanii wengine ndani ya WCB walikuwa na mpango wa kutoa albamu ila Diamond alipoweka wazi anatoa mwaka huu amebidi wampishe.

“Kiukweli mtu ambaye anatucheleweshea foleni yetu ni Chibu tu kwa sababu ni mtu wa kwanza alipata idea ya kutoa albamu mwaka huu tulikuwa tunaheshimu wazo lake sisi tukawa wa pili” amesema.

Ameendelea kwa kusema Diamond alipoweka wazi namna atakavyouza albamu yake ndipo akaamua na yeye kutoa ili auze kwa watu wake wasikilize muziki wake.

“’Kwa hiyo nilikuwa na wazo la kutoa kwa mwaka huu, nilikawa nataka yeye atoe na mimi nitoe na wengine wote watoe, watu kibao wana mangoma ndani” amesisitiza.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)