Haya si maneno yangu bali ni maneno ya Mganga wa Jadi kutoka nchini Tanzania ajulikane kama MUNGWA KABILI.
Dokta. MUNGWA KABILI aliyasema maneno hayo hivi karibuni, alipokuwa akifanya mahojiano ya moja kwa moja kwenye kituo kimoja cha redio kilichopo jijini Mombasa nchini Kenya.
Maneno ya Dokta Mungwa yalikuja mara baada ya mwanamama mmoja kutoka Malindi Kenya kupiga simu akielezea alivyo jawa na hofu kubwa kwa sababu usiku wa kuamkia siku hiyo, bundi walitua kwenye mti ulio kuwa kwenye nyumba iliyo jirani yake na kutoa vilio vya uchuro kwa masaa mawili.
Dokta Mungwa Kabili alikuwa na haya ya kusema :
Pole sana dada angu kwa masaibu yaliyo kukuta, lakini hata hivyo usiwe na hofu kwa sababu, si kila mlio wa bundi una maanisha uchuro. Wakati mwingine bundi hutoa sauti kumaanisha kitu tofauti kabisa lakini kwa sbabu watu wengi tumeshajiaminisha kuwa kila bundi aliapo ni uchuro basi tunapotokea na hali hiyo hujawa na hofu kama ilivyo kutokea wewe.
Kitu kimoja cha hakika ninacho penda kukujulisha ni kwamba, siku yoyote utakayo pata kusikia sauti ya bundi, basi jua kuwa umesikia sauti hiyo kwa sababu bundi wenyewe ndio wametaka wewe usikie sauti yao. Hii maana yake nini ? Maana yake ni kwamba, kuna ujumbe ama ishara fulani ambayo bundi wanataka uipate.
Katika ndege wote walio umbwa na Mwenyezi Mungu, bundi ndio ndege pekee mwenye uwezo wa kuruka,kupaa na kutua bila kupiga kelele wala kutoa sauti yoyote ile. Mungu ameya dizaini mabawa ya bundi katika namna ya kipekee, namna inayo mfanya bundi aweze kupaa bila kupiga kelele pamoja na kwamba, kwa kufanya hivyo huku’nguta mbawa zake.
Bundi anaweza kutua kwenye paa la nyumba yako, akakaa hadi alfajiri na kuondoka pasi na wewe kujua.
Ukiona umesikia sauti ya bundi, basi tambua ni bundi mwenyewe ndio amekusudia usikie sauti yake kwa sababu kuna ujumbe maalumu anataka kukupa.
Wachawi wanamfahamu vizuri sana bundi ndio maana wanampenda sana wala hawashitushwi na mlio wake.
Wachawi wanampenda sana bundi kiasi cha kuiga karibu tabia zote za ndege huyu wa usiku.
Baadhi ya tabia za bundi ambazo wachawi wameziiga ni pamoja na:
1. Bundi ndio ndege pekee ambae huwa hapigi kelele anapokuwa anapaa na kutua. Ndege wengine wote huwa wanapiga makelele pindi wanapokuwa wanapaa kwa sababu ya kupiga mabawa hali ambayo ni tofauti kwa bundi. Bundi hupaa kimya kimya na hutua kimya bila mawindo yake kujua. Hii inatokana na jinsi Mungu alivyo ya dizaini mabawa na manyoya yake ili viweze kumsaidia kupata ridhiki yake ya kila siku. Wachawi wanapokuwa wanafanya mipango yao ya kichawi hufanya kimya kimya bila watu wengine kujua. Na huwa hawataki kabisa kujulikana.
2. Bundi hutaka sauti yake isikike pale tu anapo amua isikike. Unaposikia sauti ya bundi jua umeisikia kwa sababu ametaka uisikie na wala si vinginevyo . Vivyo hivyo wachawi pia hutaka nguvu zao au mambo yao yajulikane pale tu wanapotaka vijulikane na si vinginevyo.
3. Bundi huanza kuruka usiku giza linapo ingia. Vivyo hivyo wachawi huanza shughuli zao usiku pindi giza linapo ingia.
4. Sio kwamba bundi hawawezi kuruka mchana . Wakati mwingine bundi huruka mchana kutafuta mawindo yao na hufanya hivyo pindi kunapo kuwa na sababu ya msingi kama vile kutafuta chakula hasahasa katika kipindi ambacho wanakuwa na upungufu wa chakula au hawakupata mawindo ya kutosha wakati wa usiku.
Vivyo hivyo wakati mwingine wachawi hulazimika kufanya baadhi ya shughuli zao nyakati za mchana ingawa uchawi unao fanyika usiku huwa na nguvu kubwa zaidi kuliko unao fanyika mchana.
5. Bundi hupenda kufanya shughuli zao usiku wakati mawindo yao yamelala, vivyo hivyo wachawi hupenda kufanya shughuli zao usiku wakati wahanga wao wamelala.
6. Bundi huwa hawajengi vichali vyao wenyewe na badala yake hutumia vichali vya ndege wawindao mchana kama vile mwewe, fundi chuma na kunguru. Vivyo hivyo wachawi huwa hawaishi kwenye nyumba walizo jenga kwa jasho lao wenyewe. Huishi kwenye nyumba zilizo jengwa na watu wengine, na wao huzimiliki kwa kutumia nguvu ya uchawi.
Kama hiyo haitoshi ,wachawi huwa hawahifadhi majini wabaya kwenye miili yao wenyewe. Hutumia miili ya watu wengine kuhifadhi majini na mapepo wachafu. Wakati mwingine unaweza kuwa na mapepo wachafu sio kwa sababu kuna watu wamekutumia ili upate madhara ila kwa sababu wachawi wanatumia mwili wako kama kibanda cha kufugia na kutunzia majini yao.
7. Wakati mwingine bundi hulana wao kwa wao. Bundi wakubwa wenye pembe kubwa huwala bundi wa saizi ya kati na bundi mbilikimo vivyo hivyo bundi wa saizi ya kati hula bundi mbilikimo isipokuwa bundi mbilikimo ndio hawana uwezo wa kuwala bundi wengine. Vivyo hivyo wachawi hutoa sadaka zap watoto wao , waume,wake , wazazi na ndugu zao.
8. Kwa kawaida bundi huishi hadi miaka kumi . Bundi hutaga mayai matatu hadi manne na huatamia mayai kwa wiki tatu hadi nne. Wanapototoa watoto, bundi mbilikimo huwalisha makinda yao kwa siku 27 wakati bundi wa saizi ya kati na wale bundi wakubwa wenye mapembe makubwa huyalisha makinda yao kwa muda wa siku 70. Wanapokuwa wanayalisha makinda yao, huyalisha kwanza makinda yenye afya na nguvu kisha hufuata makinda dhaifu. Hii maana yake ni kwamba, kama hakuna chakula cha kutosha, basi makinda yaliyo dhaifu yatakufa kwa njaa. Vivyo hivyo wachawi katika kafara zao huwa wanatoa kafara zilizo nona kwanza kisha hufuata kafara dhaifu.
9. Bundi hawaoni vitu vya karibu, huona vitu vya mbali tena mbali sana. Vivyo hivyo Wachawi kwa kutumia rada zao za kichawi wanaweza wasijue kesho utapatwa na nini lakini wanaweza kujua utakuja kuwa nani baada ya miaka ishirini ijayo. Ndio maana huweza kuiba nyota za watu wakingali wachanga.
10. Ukiachilia mbali nyani na sokwe, bundi ndio kiumbe mwenye sura inayo fanana sana na sura ya mwanadamu. Hii ni kwa sababu macho ya bundi yamekaa kama ya mwanadamu. Macho ya bundi yamekaa kwa mbele na yanaona kitu kimoja kwa wakati mmoja ilihali ndege wengine macho yao yamekaa pembeni kulia na kushoto na yanaona vitu viwili kwa wakati mmoja, yani jicho la kulia linaona kitu kingine na jicho la kushoto linaona kitu kingine kwa wakati mmoja.
Kwa sababu hii Mungu amempa bundi shingo yenye uwezo wa kuzunguka mbele nyuma . Unapopita kwenye mti ambao bundi ametua atakutazama, ukimpita katika usawa wake wa machoi atageuza macho yake na kukutazama hadi mwisho wako. Wachawi pia hufanya vivyo hivyo. Unapowapita katika vijiwe vyao,watakutazama hadi utakapo malizikia.
11. Bundi hufumba macho kama mwanadamu yaani kutoka juu kwenda chini tofauti na ndege wengine wote ambao wao hufumba macho kutoka chini kwenda juu.
Na Sio kweli kwamba bundi hawaoni mchana, bundi wanaona mchana vizuri sana tu, ila kwa sababu macho yao ni makubwa na makali sana yenye uwezo wa kuona mara saba zaidi ya mwanadamu, usiku kwao huwa kama mchana kwetu ndio maana hupendelea zaidi kuwinda usiku. Wachawi hutoka usiku kuwanga sio kwa sababu hawaoni mchana. Hufanya hivyo kwa kumuiga bundi.
12.Bundi anapokutana na hatari hutuna na kuwa mkubwa mara mbili ya ukubwa wake wa asili. Mchawi anapokutana na changamoto yoyote katika shughuli zake za kichawi huenda kutafuta msaada kwa wachawi wenye uwezo mkubwa mara mbili zaidi yake.
13.Bundi huwa na mkia mfupi sana kiasi kama huwajui bundi ukimuona kwa ukaribu zaidi kwa mara ya kwanza unaweza kudhani mkia umekatwa. Wachawi huwa na mawazo mafupi sana. Mfano Wachawi hutumia mkia wa bundi kufanya shughuli mbalimbali za kichawi kama vile kufupisha maisha ya maadui zao, au kufunga maumbile ya kiume yawe mafupi, kufunga mahusiano yawe mafupi nakadhalika.
14. Pamoja na kwamba bundi wana tofautiana ukubwa wa maumbile, yaani wakubwa, saizi ya kati na wadogo ama bundi mbilikimo, lakini bundi wote wana sifa zinazo fanana, mfano bundi wote huwa na vichwa vikubwa kuliko maumbile yao, wote wana manyoya laini, wote huwa na mikia mifupi sana, wote huwa na rangi ima ya kahawia au ya kijivu , huwa na milio inayo fanana, huruka na kupaa kimya kimya, huwa na manyoya kwenye miguu. Vivyo hivyo wachawi pamoja na kwamba, wanaweza kuwa na nguvu na madaraja tofauti katika uchawi,lakini wote huwa na tabia zinazo fanana kama vile chuki, husda, unafiki , roho ya mbaya,mawazo mafupi nakadhalika.
15. Pamoja na kwamba bundi wote huanza kutafuta mawindo yao pindi giza linapoingia, lakini hutoka kwa nyakati tofauti tofauti. Mara nyingi huanza kutoka bundi mbilikimo. Hawa bundi mbilikimo hasa wale wanaoishi porini hutoka kuanzia saa 4 usiku, bundi wa saizi ya kati hutoka kuanzia saa sita usiku na bundi wenye pembe kubwa hutoka kuanzia saa nane za usiku . Wachawi nao wanapo kuwa wanaenda kuwanga na kufanya shughuli zao za kichawi nyakati za usiku hupishana nyakati. Ingawa vikundi vingi vya kichawi huanza kutoka kuanzia saa sita usiku, lakini hupishana. Vingine hutoka saa saba , vingine saa nane. Tofauti ni kwamba karibu wachawi wote hurudi majumbani mwao nyakati sawa.
Hata hivyo, bundi hutoka kwa nyakati tofauti kwa sababu maalumu. . Bundi karibu wote wakubwa kwa wadogo hushea vichali na huishi katika eneo moja. Hutoka kuwinda nyakati tofauti tofauti kwa ajili ya kupunguza ushindani wakati wa mawindo..
16. Pamoja na kwamba macho ya bundi yana nguvu sana lakini wanapokuwa katika mawindo hutumia zaidi masikio yao kuliko macho yao. Masikio ya bundi yana nguvu sana na huweza kusikia hata sauti ya kitu kilicho umbali mrefu sana. Hata hivyo bundi wanapokuwa wanaenda kuwinda wakati wa mchana hutumia macho zaidi kuliko masikio. Vivyo wachawi, huamini zaidi vitu wanavyo visikia kuliko wananvyo viona. Yaani mchawi kila anacho ambiwa kuliko kile alicho kiona. Kwa mfano wewe A una ujauzito hata wa miezi sita. Lakini kwenye kilinge cha wachawi alipoenda kukuroga ,ukapewa jina kuwa wewe ni MGUMBA. Basi mchawi ataendelea kukuita na kukuchukulia na kuamini kuwa wewe ni mgumba. Ataendelea kuamini hivyo hata kama utazaa watotyo kumi.
17. Bundi wanapokuwa wanapaa huutawala upepo na anga. Wana mamlaka juu ya anga , na upepo. Vivyo wachawi wanapo kuwa wanapaa huamini kuwa wana mamlaka juu ya anga na upepo kama alivyo bundi.
18. Bundi huzungusha kichwa kupima umbali wa anapotaka kuruka vile vile wachawi hupima nguvu ya kiroho ya mtu kabla ya kumtupia uchawi.
19. Ukiachilia mbali bundi wanao kula wadudu, bundi wengi huwa hawana tabia ya kuhama hama. Wanaweza kukaa katika eneo moja kwa zaidi ya mwaka mmoja. Wachawi pia huwa hawami hami. Huweza kukaa katika mtaa mmoja kwa zaidi ya miaka arobaini. Na wanapokuwa wanatengeneza uchawi wa kuwatuliza wanaume kimapenzi hutumia vichali vya bundi walio kaa kwenye kichali hicho kwa muda wa mwaka mmoja na zaidi.
20. Wakati mwingine bundi hupenda kuwinda wadudu wanao tembea usiku ili kuwa na uhakika wa kupata kitoweo. Wadudu hao ni popo. Vivyo hivyo wachawi wakati mwingine hufanya ulozi nyakati za usiku katika maeneo au mazingira ambayo walengwa wao wanakuwa macho ili kuwa na uhakika wa kupata mawindo yao. Mfano ni kwenye klabu za usiku zinazo kesha, kwenye misiba au sherehe zinazo kesha nakadhalika
21. Tunafahamu kuhusu uwepo wa bundi pindi wanapo toa milio na sio pindi wanapokuwa kimya. Vivyo tunafahamu kuhusu uwepo wa wachawi katika mazingira tunayo ishi pindi wanapo tupa uchawi wao na sio wanapokuwa hawajatupa uchawi.
22. Bundi wakubwa hutoa sauti kubwa kuliko bundi wadogo. Vivyo hivyo, wachawi wadogo hujulikana zaidi kuliko wachawi wakubwa.
KWANINI WACHAWI WANAMPENDA SANA BUNDI
Wachawi wanampenda sana bundi kwa sababu wana amini bundi ni kiumbe mwenye faida nyingi sana kwao. Baadhi ya mambo ambayo wachawi huya amini kama faida zinazo letwa na bundi ni kama ifuatavyo :
1.Bundi huwasaidia wachawi kuchunga misukule yao ; Katika ulimwengu wa wachawi mtu aliye chukuliwa msukule mara baada ya kukatwa ulimwi hatua inayo fuatwa huwa ni kulishwa vumbi la mifupa iliyo temwa na bundi. Dawa hiyo huufanya msukule huo usahau kila kitu ulichokuwa unakijua kabla ya kuchukuliwa msukule.
Kwa wasio fahamu, bundi huwa wanakula wadudu na wanyama mbalimbali kama vile nyoka, nge,panya, pimbi, panyabuku, ndezi, popo na hata samaki. Bundi huwa wanakula vitu vizima vizima na kutema mifupa yao. Sasa hii mifupa inayo temwa na bundi ndio wanayo itumia wachawi kuwalisha misukule wao kwa minajili ya kuwafanya wasahau kila kitu walichokuwa wanakijua kabla hawaja chukuliwa msukule pamoja na kuwapa uwezo wa kuona mambo yasiyo onekana na kutokuonekana na watu wa kawaida.
2. Bundi huwasaidia wachawi kulinda mashamba yao dhidi ya wadudu waharibifu wa mazao
Moja kati ya shughuli kuu za wachawi ni kilimo kwa kuwatumia misukule. Kwenye mashamba huwa kunakuwaga na panya waharibifu wa mazao . Na kama nilivyo sema hapo mwanzo kuwa, moja kati ya yakula vinavyopendwa sana na bundi ni panya. Kwa wastani bundi mmoja anaweza kula hadi panya elfu moja kwa mwaka. Mchawi akiwakaribisha bundi ishirini kuwa wanatembelea kila siku shambani kwake maana yake ni kwamba ndani ya mwaka mmoja watakuwa wamemsaidia kula panya elfu ishirini ambao wanaweza kuharibu hadi tani 31 za mazao.
Hivyo basi kwa wachawi hapo bundi huwa msaada wao mkubwa wa kiuchumi. Huwasaidia kutunza na kulinda mashamba yao dhidi ya wadudu waharibifu. Huwasaidia kuokoa gharama za kununua dawa za kuua wadudu waharibifu ambazo zingeweza kuwagharimu mamilioni ya shilingi.
3.Bundi huwasaidia wachawi kuondokana na madhara ya wadudu hatari kama nyoka na nge
Bundi ni walaji wazuri sana wa wadudu hatarishi kwa binadamu kama vile nyoka na nge. Hivyo kwa mchawi kuwakaribisha bundi shambani kwake au nyumbani kwake anakuwa amejihakikishia kuwa hawezi kupatwa na madhara ya kuumwa na nyoka au nge kwa sababu bundi wanapoweka makazi yao katika eneo lolote lile, nyoka hawawezi kukaa mahali wapo.
4. Bundi huwasaidia wachawi katika shughuli mbalimbali za kichawi.
Kwa kutumia maarifa ya kichawi, wachawi humtumia bundi katika shughuli mbalimbali zap kichawi kama vile :
i. Kwenda kuzimu : Bundi ni mesenja wa kuzimu na dunia. Huchukua habari za kuzimu na kuzileta duniani na habari za duniani huzipeleka kuzimu . Bundi ni daraja linalo unganisha kuzimu na duniani. Ni daraja linalo unganisha ulimwengu usio onekana na ule unao onekana. Kwa wale wasio fahamu, umbali kutoka duniani na kuzimu ni kilomita sifuri. Moja kati ya mawakala wa malango makuu yanayo unganisha dunia na kuzimu ni huyu ndege aitwae bundi.Ukaribu na urafiki wa wachawi kwa ndege huyu unawanufaisha wachawi na kuzimu
ii. Kuiba na kuharibu nyota za watu hususani watoto wachanga : Wanapokuwa katika mchakato wa kuiba nyota za watu hususani watoto wachanga, wachawi humtumia bundi kufanikisha mchakato.
KWANINI WANAMTUMIA BUNDI : Bundi ana sifa moja kubwa sana. Hana uwezo wa kuona vitu vya karibu lakini ana uwezo wa kuona vitu vya mbali sana. Hiyo ni sifa yake katika ulimwengu wa nyamja ambayo ina sadifu sifa na uwezo wake katika ulimwengu wa roho. Katika ulimwengu wa roho bundi ana uwezo wa kuona na kujua mambo yatakayo mtokea mtu miaka 30 hadi sitini ijayo.
Bundi anaweza kuona kifo cha mtu miaka kumi mbele, siku moja mbele, siku mbili mbele, wiki nakadhalika.
Hii ndio sababu inayo mfanya bundi kutoa taarifa kwa mhusika, ndugu, jamaa na marafiki zake siku kadhaa kabla ya kifo cha mtu huyo.
Bundi hufanya hivyo kwa kutoa mlio maalumu. Wachawi kwa sababu wanafundishwa namna ya kuwasiliana na bundi, bundi anapotoa mlio wa kuashirikia kutokea kwa msiba, mchawi na yeye hupiga mluzi ima kwa mdogo ima kwa filimbi ya kichawi kumjibu bundi, na bundi asipo jibu mlio huo, basi mchawi anakuwa amejua kuwa siku zake zap kuishi hapa duniani zimefika ukingoni.
Mtoto anapozaliwa, wachawi kwa kutumia uchawi na nguvu za kiroho zap bundi hupeleka jina la mtoto huyo ili kujua atakuwa nani baadae, na endapo itajulikana kwamba mtoto huyo atakuwa mtu mkubwa mwenye mafanikio, basi nyota yake itaibwa mara moja.
Nyota hii inapochukuliwa ima, huuzwa kwa mtu, hutumikishwa msukule, ama kuzikwa.
Nyota ya mtoto mchanga inapo chukuliwa, hubadilishwa na nyota chafu na matokeo yake mtoto huyu anaanza kuishi maisha ambayo si yake.
Vile vile kwa kumtumia bundi, wachawi huweza kurudisha nyuma jambo baya ambalo lingemtokea mtu miaka ya mbeleni.
Kwa mfano ramani yako ya maisha inaonyesha kuwa utafariki kwa maradhi ya kisukari ukiwa na miaka 75. Wachawi kwa kumtumia bundi wanaweza kuyarejesha nyuma maradhi hayo na kukufanya uyapate ukiwa na miaka thelathini.
Mambo mengine ya kichawi ambayo wachawi huwatumia bundi kuyafanya ni pamoja na :
1. Mavi ya bundi hutumika kwenye ungo wa kusafiria kichawi
2. Mavi ya bundi huchanganywa na mavi ya chatu, sokwe, nyani, maji ya maiti, mavi ya mtu aliye jisaidia akiwa porini pamoja na madawa mengine, katika kumtia mtu mikosi.
3. Matambiko ya biashara na madini migodini
4. Hutumika kufungua milango ya kuzimu wakati wa kuvuka kutoka duniani kwenda kuzima kwa njia ya kupitia baharini.
5. Kuwa na uwezo wa kuona wachawi, kuona mambo yaliyo jificha, mambo yatakayo tokea mbeleni, mambo ya siri.
6. Kuwakaribisha watu kwenye malango makuu ya kichawi,ya miji, nchi nakadhalika.
ANAPOKUWA NCHINI TANZANIA, DOKTA. MUNGWA KABILI ANAPATIKANA KWA SIMU NAMBA
0744 000 473
ULIPITWA NA HII.?WANANCHI WAMCHAPA VIBOKO DAKITARI