ABILIA ADAI FIDIA BAADA YA KUAMSHWA GHAFLA NDANI YA NDEGE

Admin
By -
0
Abiria mmoja aliyekuwa anasafiri na Shirika la ndege la Urusi (Russian airline Aeroflot) amelitaka shirika hilo kumlipa kiasi cha Euro elfu 13 sawa na Tsh 35 baada ya kuamshwa ghafla na wahudumu wa kwenye ndege kwa ajili ya chakula.



Abiria huyo, Lev Levchenko amesema kuwa makelele hayo yalimtoa kwenye usingizi na alichoka kutokana na mfululizo wa vikao, hivyo amelitaka shirika hilo kufidia usingizi wake ili iwe fundisho kwa wengine.

“Nilichoka sana kwani nilitoka kwenye vikao vya kikazi halafu nimepumzika ghafla nasikia sauti za vijiko huku mtu ananiamsha nilishikwa na ghadhabu na hili liwe fundisho kwa wahudumu wote wa ndege nchini (Urusi)“ amesema Lev Levchenko kwenye mahojiano yake na gazeti la Daily Mail.

Hata hivyo wahudumuwa wa ndege hiyo licha ya kukalipiwa waliomba msamaha na kuendelea kuhudumia.

Shirika hilo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo kupitia mtandao wake na kudai kuwa tayari limeanza mazungumzo ya kuona namna ya kumalizana na Bwana Lev Levchenko ambaye alikuwa anatokea mjini Sochi kuelekea Moscow na ni mfanyabiashara mkubwa nchini humo.




Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)