Header Ads Widget

NDEGE YAPITILIZA YATUA ZIWANI


 Ndege ya Shirika la Ndege la West Atlantic ilipitiliza njia jana wakati ikijaribu kutua katika uwanja wa Ndege wa Montpellier nchini Ufaransa, na hatimaye kusimama pembeni mwa Ziwa.


Ndege hiyo ya mizigo aina ya Boeing 737 ilikuwa na watu watatu na wote waliokolewa na kutoka bila majeraha.

Uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo unaendelea, huku mamlaka ya anga nchini humo ikitangaza kufungwa kwa uwanja huo kwa muda usiojulikana mpaka hapo Ndege hiyo itakapoondolewa.

Post a Comment

0 Comments