SAFARI YANGU YA AFRIKA KUSINI SEHEMU YA 5

Baada ya kugonga mlango Kisha ukafunguliwa aliyefungua alikua Ni mtoto wa kike 
"Nikamwambia Naitwa Steven Ni rafiki wa Frank kutoka Tanzania" akajibu sawa ngoja nimwite Frank
Lakini chaajabu alirudi yule mwanamke na kunijibu Frank hayupo na hakai maeneo hayo kwa Sasa alihama kitambo

Ananijibu hivi wakati nimeisikia sauti ya Frank lakini ananijibu hayupo. Nikajua tayari nimesha telekezwa nikamwambia mbona Kama nimemsikia? Akajibu kuwa mwelewa Frank haishi hapa alihama kitambo akaenda mbali na kusema niondoke ataniitia Polisi


Basi nikawa Sina jinsi ikabidi niondoke huku sijui wapi nakwenda maana Mimi Ni mgeni na Sina mtu mwingine ninaemfahamu pengine atanisaidia


Nikiwa natembea njiani ghafla wakatokea vijana wasili waliokuwa wamenyoa upara ambao walikuwa wanakuja mbele yangu. Wakawa Kama wanapunguza mwendo huku wakinikalibia Kisha mmoja wa hao vijana akatoa bastola na kuniwekea kichwani.

Ilikuwa mala yangu ya Kwanzaa kuiona bastola live nilipatwa na hofu kipindi hicho wakiniamulu nitoa kila nilicho nacho mmoja akachukua begi langu pamoja na Simi yangu


Wakaniacha Kama hatua tano mmoja akarudi akanipatia passport yangu tu vingine vyote wakachukua moyoni nilishukuru kwa kuachiwa passport yangu maana ndiyo kitu muhimu zaidi kwangu kwa wakati ule


Nikabaki nimechoka nimekaa chini huku nikichukia Safari yangu ya Afrika kusini maana Frank kanikana na wahuni wameniibia


Ilikuwa mida ya saa tatu hasubui njaa Sasa ikawa inaanza kuniuma na vibaka walikuwa wamenichukulia kilakitu ilikuwa siku ngumu kwangu ambayo sita isahau kwenye maisha yangu

Nikawa natembea tu nikielekea katikati ya mji ghafla nikakutana na mtu mmoja ambae alikuwa raia wa Kenya aliponiona tu akajua Mimi Ni Mtanzania....ITAENDELEA

Post a Comment

Previous Post Next Post