Header Ads Widget

Hiki ndicho chanzo Cha vurugu palestina


 Jerusalem imekuwa ikigonga vichwa vya habari kufuatia ghasia ambazo zimekuwa zikiripotiwa mjini humo kati ya Wapalestina na vikosi vya usalama vya Israeli ambazo zimewaacha mamia wakijeruhiwa mbali na mshambulizi ya kulipa kisasi kutoka pande zote mbili yakiripotiwa.

Ghasia hizo ziliongezeka siku ya Jumatatu usiku baada wanamgambo wa Kipalestina kurusha roketi kutoka ukanda wa Gaza hadi Jerusalem.

Kundi la wanamgambo la Hamas limetishia kuwashambulia maafisa wa polisi wa Israel baada ya mamia ya Wapalestina kujeruhiwa katika eneo takatifu la Waislamu mjini Jerusalem siku ya Jumatatu.

Likijibu, Jeshi la Israel lilifanya mashambulizi ya angani dhidi ya ngome za wanamgambo katika ukanda wa Gaza.

Maafisa wa afya wa Palestina katika eneo la Gaza wanasema kwamba watu 22 wakiwemo watoto waliuawa katika shambulio hilo.

Jeshi la Israel limesema kwamba takriban wanachama 15 wa kundi la Hamas linalotawala Gaza ni miongoni mwa waliokufa.

Roketi zilirushwa kutoka Gaza hadi Jerusalem siku ya Jumatatu

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Roketi zilirushwa kutoka Gaza hadi Jerusalem siku ya Jumatatu

Siku ya Jumanne, Shirika la haki za kibinadamu la Palestina Red Crescent, liliripoti kwamba zaidi ya Wapalestina 700 walijeruhiwa katika ghasia hizo na maafisa wa usalama wa Israel mjini Jerusalem na eneo la West Bank.

Hizi hapa sababu tatu zilizopelekea kuzuka kwa mzozo huo.

1. Siku ya kusherehekea Jerusalem

Jerusalem imeshuhudia ghasia ambazo hazajiwahi kutokea tangu wikendi ya 2017, zikisababishwa na jaribio la muda mrefu la Wayahudi kujaribu kunyakua nyumba za familia za Kipalestina katika eneo lililonyakuliwa na Israeli la mashariki mwa Jerusalem.

Ghasia hizo za Jumatatu zilizuka nje ya msikiti wa Al Aqsa , katika mji wa zamani wa Jerusalem.

Wapalestina waliwarushia mawe maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia kutoka Israel ambao nao walijibu kwa kuwarushia risasi bandia za mipira na vitoa machozi .

Shirika la haki za kibinadamu la Palestina Red Crescent lilisema siku ya Jumatatu kwamba zaidi ya watu 300 walijeruhiwa.

Vikosi vya polisi vya Israel vilisema kuwa idadi kubwa ya maafisa wa polisi ilijeruhiwa pia.

Zaidi ya Wapalestina 300 walijeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Jumatatu

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,

Zaidi ya Wapalestina 300 walijeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Jumatatu

More than 300 Palestinians were injured during Monday's clashes in Jerusalem.

Msikiti wa Al Aqsa upo katika eneo takatifu linalojulikana na Waislamu kama Haram al Sharif, na Hekalu la Mlimani kwa Wayahudi.

Vikosi vya polisi wa Israel vilisema kwamba maelfu ya Wapalestina waliweka vizuizi katika eneo hilo wakitarajia kutokea kwa ghasia wakati wa maandamano ya Kiyahudi siku ya Jumatatu ili kuadhimisha siku ya Jerusalem.

Maandamano hayo yanaadhimisha hatua ya Israel kunyakuwa eneo la mashariki la Jerusalem 1967 , wakati wa vita vya siku sita ambapo ilifanikiwa kuchukua udhibiti wa mji wote.

Mji huo wa zamani upo mashariki mwa Jerusalem , ikiwa ni nyumbani kwa baadhi ya maeneo matakatifu ya kidini duniani ikiwemo: Msikiti wa Al-Aqsa, Hekalu la mlimani, Ukuta wa magharibi wa dini ya Wayahudi na kanisa la Wakristo la mtakatifu Sepulcher.

Na eneo hilo linatambulika kuwa mji mtakatifu na Wayahudi, Wakristo na ni mji wa tatu mtakatifu katika Uislamu.

Hatma ya eneo la Jerusalem mashariki ndio kiini cha ghasia kati ya Israeli na Wapalestina na kila upande unapigania haki yake.

Israel inasema kwamba eneo lote la mji huo ni mji wake mkuu , ijapokuwa hilo halitambuliwi na jamii ya kimataifa , na Wapalestina wanadai kwamba eneo hilo ndio mji mkuu wa taifa la Kipalestina litakaloundwa katika siku zijazo.

Wakati wa maandamano hayo ya kuadhimisha siku ya Jerusalem, mamia ya vijana wa Israel walipeperusha bendera na kuelekea katika maeneo hayo ya Waislamu , wakiimba nyimbo za kizalendo.

Wapalestina wengi wanachukulia hatua hiyo kama uchokozi.

Polisi wa Israel walitembelea eneo hilo kuamua kuwapiga marufuku Wayahudi wakati wa maadhimisho ya siku ya Jerusalem.

Maandamano ya kuadhiisha siku ya Jerusalme yanaadhimishwa kufuatia hatua ya Israel kunyakua mji huo

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Maandamano ya kuadhiisha siku ya Jerusalme yanaadhimishwa kufuatia hatua ya Israel kunyakua mji huo

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitetea ulinzi uliowekwa.

"Hii ni vita kati ya wavumilivu na wasio na uvumilivu, kati ya wasiofuata sheria na wanaofuata sharia," alisema.

"Wale wanaotaka kuchukua haki zetu mara kwa mara hutulazimisha kusimama kidete, kama maafisa wa polisi wa Israeli wanavyofanya."

Kwa upande wake rais wa Palestina Mahmoud Abbas alishutumu vitendo vya Israel.

"Shambulio la kinyama la vikosi vya Israel dhidi ya waumini waliokuwa katika msikiti mtakatifu wa Al Aqsa na maeneo yake ni changamoto mpya kwa jamii ya kimataifa," alisema msemaji wake Nabil Abu Rudeineh.

2.Uwezekano wa kuzifurusha familia za Wapalestina.

Wimbi jipya la ghasia linatokana na juhudi za siku nyingi za Wayahudi kuzifurusha familia kadhaa za Kipalestina kutoika katika makazi yao karibu na wilaya ya Sheikh Jarrah mashariki mwa jerusalem.

Jerusalem ilishuhudia ghasia mbaya zaidi tangu 2017

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,

Jerusalem ilishuhudia ghasia mbaya zaidi tangu 2017

Jerusalem

IMAGE SOURCE,EPA

Caption,

Jerusalem experienced the worst fighting of its kind since 2017.

Umauzi wa mahakama mwaka huu uliounga mkono kufurushwa kwao ulizua shutuma kutoka kwa Wapalestina.

Mahakama ya kilele nchini Israel ilikuwa inatarajiwa kusikiliza kesi siku ya Jumatatu lakini kikao hicho kikaahirishwa kutokana na ghasia hizo.

3. Hali ya hofu wakati wa Ramadhan

Wimbi hili la ghasia linajiri katika siku za mwisho za mwezi mtukuafu wa Ramadhan.

Kizuizi cha Ramallah

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Hofu ilitanda tangu kuanza kwa mwezi wa Ramadhan katikati ya mwezi Aprili , huku kukiwa na msururu wa matukio ambayo yamesababisha ghasia.

Wakati Ramadhan ilipoanza , ghasia za usiku zilizuka kati ya polisi na Wapalestina wakipinga vizuizi vilivyoweka nje ya lango kuu la Damascus katika mji wa zamani wa Jerusalem ambalo lilikuwa limewazuia kukongamana eneo hilo usiku kucha.

Lakini ghasia hazikutokea Jerusalem pekee kwani sehemu nyengine pia zilirekodiwa katika mji wa Haifa , Kaskazni mwa Israel na mji wa karibu wa Ramallah katika eneo la West Bank.

Wapatanishi wa mashariki ya kati , wakiwemo Marekani, muungano wa Ulaya, Urusi na Umoja wa Mataifa wameonyesha kukerwa na ghasia hizo na kutoa wito kwa pande husika kuvumiliana.

Post a Comment

0 Comments