SAFARI YANGU YA AFRIKA KUSINI SEHEMU YA 6

Akaniuliza wewe Ni Mtanzania? Nikamjibu ndiyo Mimi Ni Mtanzania 
Akaniuliza unaishi wapi? Nikamjibu Sina pakuishi nikamwelekeza madhira yote yaliyonikuta


Baada ya kumwelezea akaniambia kuwa yeye Ana nyumba amepanga yeye na rafiki yake kwahiyo twende huko tukaishi wote na akanihaidi kupata kazi

Kweli tuliongozana mpaka alipopanga mtaa unaitwa hilbrow tulipofika tukamkuta rafiki yake. Akanitambulisha kwa rafiki yake na rafiki yake akanielewa vizuri akanikaribisha


Kipindi chote hicho hakuniambia kuwa anafanya kazi gani akaniangalia chakula nikala tukawa tunatazama TV

Baada ya muda kidogo nikamuuliza bro unafanya kazi gani? Akaninijibu usiwaze kuhusu kazi yangu muda ukifika utajua kilakitu Wala usiwe na hofu

Baada ya muda kidogo akaondoka akarudi na Pombe na soda tukanywa ndipo akaniambia kazi aliyokuwa anaifanyia


Akasema hawana kazi rasmi wao Ni wezi wanaiba vitu na hata pesa na akasema atafurai na Mimi nikijiunga nao katika shughuli zao za wizi


Nikabaki nimechoka na sikuwa na jinsi nikajikuta nimekubali kujiunga nao kwaajili ya kufanya wizi ili nipate pesa ya kuendesha maisha ingawa sikuvutiwa Ila ilinibidi iwe Ivo

Nikamuuliza wizi wanao ufanya niwizi wa namna gani? Akaniambia huwa wanaiba kwenye maegesho ya magari na kwa wahindi na wazungu maana huwa na Mali nyingi. Ilipofika usiku majira ya saa tano akaniambia huu ndiyo muda wa kwenda kazini..... ITAENDELEA

Post a Comment

Previous Post Next Post