
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza rasmi matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita wa mwaka 2025, uliofanyika kuanzia Mei 5 hadi 26, 2025.
Taarifa imetolewa leo, Jumatatu, Julai 7, 2025, visiwani Zanzibar, na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza la mtihani Tanzania Necta, Profesa Said Mohamed.
Mtihani huu uliwashirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchini, ambapo walifaulu wanapata nafasi ya kusonga mbele kwa elimu ya juu (vyuo vikuu) au vyuo vya kato.
Kwa miaka ya karibuni Baraza la mtihani Tanzania (NECTA) lilifuta utaratibu wa kutangaza wanafunzi bora na shule bora zilizofanya vizuri.
Hii ili ilifanywa kwa maelezo kuwa walikuwa baraza lilikuwa linataka kuleta usawa na kupunguza hali ya baadi ya shuke kuonekana ni bora kuliko shule nyingine.
Bofya Hapa Kupata Matokeo>>>
Hata hivyo wadau mbalimbali wa elimu walikosa utaratibu huo wakisema, badala ya kufuta utaratibu huo, serikali ilitakiwa kuboresha shule za umma kwa kuwa karibu miaka yote, shule na wanafunzi waliokuwa wakifanya vizuri walikuwa kutoa shule binafsi na zile zinazomilikiwa na za taasisi hasa za dini.