Raisi was Afghanistan akataa kuwaachia wafungwa was Taliban

Rais wa Afghan Ashraf Ghani amesema kuwa serikali yake haitaunga mkono kuachilia wafungwa wa Taliban kama ilivyoelezwa kwenye makubaliano waliofikia na Marekani na wanamgambo hao.
Chini ya makubaliano hayo ya kihistoria yaliyofikiwa Jumamosi hii Qatar, wafungwa 5,000 wa Taliban wataachiliwa huru katika mabadilishano ya raia karibia 1,000 wa serikali wanaozuiliwa kufikia Machi 10.
Bwana Ghani amesema kuachiliwa kwa wafungwa namna hiyo hakuwezi kufanyika kabla ya mazungumzo, bali ni lazima hilo liwe sehemu ya majadiliano.
Makubaliano ya Marekani na Taliban yanajumuisha kuondoka kwa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan kwa awamu.
Kwa mabadilishano, kundi hilo la Kiislamu lenye msimamo mkali lilikubali kufanya mazungumzo na serikali ya Afganistan.
Makubaliano hayo pia yalihakikisha kuwa Taliban inazuia kundi la al-Qaeda na makundi mengine yoyote yenye msimamo mkali kuendesha shughuli zake katika maeneo wanayodhibiti.
Marekani iliingilia Afghanistan wiki kadhaa baada ya shambulio la Septemba 2001, New York na kundi la al-Qaeda, wakati huo likiwa na makao yake Afghanistan. Kundi la Taliban lilitimuliwa madarakani lakini likawa kikosi kikubwa cha wanamgambo kiasi kwamba 2018, lilikuwa linaendesha shughuli zake kwa zaidi ya theluthi mbili ya maeneo nchini humo.

Ghani amesema nini?

Chini ya saa 24 tu baada ya makuabaliano kufikiwa Doha, rais wa Afghanistan amewambia wanahabari katika mji wa Kabul kuwa: "Kusitisha vita taratibu kutaendelea kwa lengo wa kufikia makuabliano ya kusitisha kabisa vita."
Lakini ameongeza: "Hatudhamirii kuachilia huru wafungwa 5,000''.
"Hatua hii ni haki ya raia wa Afghanistan na kupenda kwao. Huenda kukajumuishwa kwenye ajenda ya mazungumza na pande zote, lakini haliwezi kutimizwa kabla."
Mfungwa yeyote kuachiliwa huru, aliongeza, "sio kwa idhini ya serikali ya Marekani" bali "ni kwa mamlaka ya serikali ya Afghan".
Wataliban wakiribia 10,000 waliokamatwa wanazuiliwa na Afghanistan.
Ujumbe wa Marekani Zalmay Khalilzad na Taliban, Mullah Abdul Ghani BaradarHaki miliki ya pichaAFP
Image captionUjumbe wa Marekani Zalmay Khalilzad na Taliban, Mullah Abdul Ghani Baradar walisalimia kwa mkono kwenye makubaliano hayo
Maafisa wa Marekani, Afghanistan na Taliban, wote wamekuwa makini sana kutoita mkataba wa Doha makubaliano ya amani. Lakini kwa Afghanistan, matumaini yenye tahadhari yamekuwa yakiongezeka tangu ile wiki ya kukubaliana kupunguza ghasia au kusitisha kwa muda mapigano na kupelekea kusainiwa kwa makubaliano yaliofikiwa.

Tulifikaje hapa na kwanini imechukua muda mrefu?

Vita vya Afghanistan vimekuwa vya umwagaji wa damu kwa miaka mingi sasa, huku Taliban wakiendelea kudhibiti au kutafuta kutwaa maeneo zaidi ingawa bado hawajafanikiwa kutwaa maeneo muhimu vya mijini.
Na hilo limefanya pande zote kutambua kwamba hakuwa anayeweza kuibuka na ushindi wa kijeshi moja kwa moja. Wakati huohuo, Rasi Trump amekuwa muwazi kuhusu dhamira yake ya kutaka kuondoa vikosi vya Marekani nchini humo.
Moja ya mambo ya msingi yaliyozingatiwa na Marekani na kuwezesha mazungumzo ulikuwa uamuzi wa 2018 wa kubadilisha sera yake kwamba Taliban kwanza wazungumze kwanza na serikali ya Afghan ambayo kundi hilo inadai kuwa serikali iko madarakani kinyume cha sheria.
Badale yake Marekani ikiamua kufanya majadiliano ya moja kwa moja na Taliban kusikiliza matakwa yao - uwepo wa wanajeshi wa kigeni Afghanistan. Mazungumzo hayo yalitengeneza mazingira mazuri ya makubaliano yaliyofikiwa Jumamosi, huku Taliban wakikubali pia nao kushughulikia suala la sababu kuu ya kuvamia Marekani 2001, na kundi lenye kuhusishwa na al-Qaeda.
taliban team in dohaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMkuu wa kundi la Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar (katikati) alitia saini mkataba
Mkataba huu sasa umefungua ukurasa mpya wa kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na wanamgambo wa Taliban na viongozi wengine wa kisiasa wa Afghan wakiwemo viongozi wa ngazi ya juu serikalini.
Mazungumzo hayo yatakuwa changamoto zaidi. Kwa namna yoyote ile ni lazima kuwe na maridhiano kati ya maono ya Taliban ya kuwa na uongozi unaoegemea Uislamu na serikali ya Afghanistan ya sasa yenye kuendeleza demokrasia ambayo imeundwa tangu 2001.
Je hilo linaweka wapi haki za wanawake? na je msimamo wa Taliban ni upi katika suala la demokrasia? Haya ni baadhi ya maswala yatakayopata ufumbuzi tu majadiliano ya pande mbili yatakapoanaza.
Hadi kufikia sasa, pengine ni kwa kukusudia, Taliban wamekuwa wasioeleweka. Kuna vinavyoweza kuwa vikwazo hata kabla mazungumzo haya kuanza. Taliban inataka wafungwa wao 5,000 kuachiliwa huru kabla ya mazungumzo kuanza lakini serikali ya Afghan inataka kutumia wafungwa hao kama nguvu yao katika majadiliano ili kushawishi Taliban kusitisha mapigano.
Na vilevile, kuna huu mgogoro wa kisiasa unaoendelea juu ya matokeo ya uchaguzi wa urais - na Abdullah Abdullah mpinzani wa Ashraf Ghani anayedai kwamba ulikubwa na udanganyifu.
Hali ya ukosefu wa uthabiti wa kisiasa kunaweza kufanya iwe vigumu kuunda timu imara ya kufanya majadiliano wakati ambapo waangalizi wa kimataifa wanataka meza ya mazungumzo kuwakilisha kila pande ikiwemo Taliban.
US troops in Logar province, Afghanistan, July 2018Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBado haijafahamika ni wanajeshi wangapi wa Marekani watakaosalia iwapo amani itadumu
Afisa mmoja wa Afghan alikubali kwamba hata wanapotaka kuanza, kwa kigezo cha kuwakilisha kila upande hata kwa upande wa Afghan pekee, mazungumzo hayo yanaweza kuchukua miaka.
Lakini Marekani imeashiria nia yake ya kutaka kuondoa wanajeshi wake wote ndani ya kipindi cha miezi 14 iwapo Taliban watatimiza makubaliano yao.
Bado haijafahamika ikiwa hilo linamaanisha kuwa wanajeshi wa Marekani wataendelea kuwepo hata baada ya miezi hiyo ikiwa hakutakuwa kumefikiwa makubaliano yoyote.
Maafisa wa Afghanistan wamesisitiza kwamba kujiondoa ni lazima lakini mwanadiplomasia mmoja alisema kuwa, kutategemea tu na kuanza kwa mazungumzo ya ndani ya Afghan hata kama yatakuwa hayajafikia ukomo.
Alionesha wasiwasi kwamba ikiwa Marekani itaondoa wanajeshi wake na kundi la Taliban liamue kuanza tena vita bila shaka jeshi la Afhgan litakuwa katika hali tete.
Smoke rising above Kabul city after an attackHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVita vya Afghan vimedumu kwa karibu miaka 20, na mara nyingi hukumba mji mkuu wa Kabul
Wachambuzi wengine wameonya kwamba kundi la Taliban halionekani kuwa katika hali ya kutaka maridhiano lakini wanaonekana kutafuta kutambualiwa na kuhalalishwa kimataifa. Bila shaka hafla ya kutia saini makubalino na Marekani imetimiza hilo na huenda wakahisi kuwa majadiliano ndio njia nzuri ya kufikia malengo yake.
Kipaumbele kwa raia wengi wa Afghan hata kama ni kwa muda mfupi ni kupungua kwa vurugu au kumaliza kabisa vita. Hilo litafahamika wiki chache zijazo wakati watakapoanza majadiliano iwapo litatokea.

Post a Comment

Previous Post Next Post