Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mahiwa, wilaya na mkoa wa Lindi, John Ngalu (38) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya mkoa wa Lindi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake anayesoma kidato cha tano.
Hayo yalielezwa jana na wakili wa serikali, Juma Maige alipozungumza na Muungwana Blog, ofisini mwake mjini Lindi.
Maige alisema Ngalu alipandishwa kizimbani tarehe 5 mwezi huu baada ya kufunguliwa kesi ya jinai yenye namba za jalada 4/2020, na kuongeza kuwa kitendo hicho kilifanyika kwenye nyumba anayoishi mwalimu huyo. Ambayo ipo katika eneo la shule hiyo.
Alisema mshitakiwa huyo alikutwa usiku baada baadhi ya wananchi ambao ni raia wema kutoa taarifa,kwa wananchi wenzao ambao walipokwenda eneo la tukio walimkuta akifanya mapenzi na mwanafunzi wake huyo.
Maige alisema inadaiwa kuwa kitendo cha namna hiyo kwa mwalimu huyo na mwanafunzi wake ni cha muda mrefu. Hali iliyo sababisha wananchi hao wamchoke na kuamua kumkamata.
Kesi hiyo itaendelea tena tarehe 13 Februari 2020. Huku Ngalu akirudishwa mahabusu baada kushindwa kutekeleza vigezo na masharti ya dhamana.