
Usiku wa kuamkia leo juma mosi mtu mmoja ameuawa tena kibiti
tukio hilo limetokea katika kijiji nyambwanda wilayani kibiti ambapo bwana Hamis ndikanye miaka 54 ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo
ndugu wa marehemu anasema walikuja watu watano wakiwa na bunduki wakamfunga kitambaa usoni mke wa marehemu na kisha kumpiga riaasi marehemu Hamis
kwa mujibu wa mganga wa kituo cha afya kibiti alisema kuwa marehemu amepigwa risasi mbili moja kichwani na nyingine mgongoni
mpaka sasa watuhumiwa hawajajulikana na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi
Tags
Kitaifa