Idadi ya wanajeshi wa Marekani wanaougua majeraha ya ubongo kufuatia shambulio la Iran dhidi ya wanajeshi wa Marekani katika kambi moja nchini Iraq mwezi Januari imefikia 109, kulingana na maafisa wa Marekani.
Idadi hiyo iliongezeka kutoka wanajeshi 64 walioripotiwa hapo awali na Pentagon. Rais Donald Trump awali alisema kwamba hakuna raia wa Marekani waliojeruhiwa wakati wa shambulio hilo.
Shambulio hilo la tarehe 8 mwezi Januari linajiri huku kukiwa na wasiwasi kuhusu mauaji ya jenerali mmoja wa Iran. karibia asilimia 70 ya wanajeshi waliojeruhiwa wamerudi kazini , pentagon iliongezea katika taarifa.
Ongezeko la visa vilivyoripotiwa linatokana na majeraha madogo ikimaanisha kwamba dalili huchukua muda kujitokeza , Pentagon ilisema katika mkutano na vyombo vya habari mwezi Januari.
Mbunge wa chama cha Republic nchini Marekani Joni Ernst alitoa wito wa kutolewa kwa majibu zaidi siku ya Jumatatu.
''Ni muhimu kuwa na mpango wa kuwatibu hawa waliojeruhiwa'' .
"Nimetoa wito kwa Pentagon kuhakikisha usalama na utunzaji wa vikosi vyetu vilivyopelekwa ambao wanaweza kuwa na majeraha ya mlipuko nchini Iraq," aliandika katika twitter.
Mwezi uliopita Rais Trump alipuuzilia mbali uwepo wa majerha ya ubongo alipoulizwa juu ya athari ya shambulio hilo.
"Nilisikia kuwa walikuwa na maumivu ya kichwa, na mambo kadhaa, lakini ningesema, na naweza kuripoti, sio mbaya sana," alisema.
Alipoulizwa kuhusu majerha ya ubongo au TBI alisema: "Sidhani kama ni majeraha makubwa sana ikilinganishwa na majeraha mengine ambayo nimeona."


Je majaraha mabaya ya ubongo ni yapi?
Majeraha ya TBI hupatikana sana katika maeneo ya vita , kulingana na jeshi la Marekani.
Sababu kubwa ya TBI kwa wanajeshi waliopelekwa katika maeneo ya vita ni milipuko, kulingana na kituo cha Ulinzi cha Marekani kinachokabiliana na majeraha ya ubongo.
Majeraha hayo hutajwa kuwa madogo , kiwango cha kadri ama mabaya zaidi. Majeraha madogo ya TBI hutajwa kuwa mshtuko. na unaweza kusababishwa na mlipuko.
Shinikizo ya juu ya anga ikifuatiwa na shinikizo ndogo au ukosefu wa hewa. ". Ukosefu huo wa hewa unaweza kuingiza vitu hatua inayowafanya wanajeshi kuumia na hivyobasi kupata jeraha.
Zaidi ya wanajeshi 400,000 wamepatikana na TBI tangu 2000 kulingana na serikali ya Marekani.
Tags
Kimataifa

