Matayarisho yanaendelea kwa kasi katika shule ya Kabarak, kwenye boma la aliyekuwa rais Daniel arap Moi.
- Zaidi ya watu 10,000 wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya rais mstaafu Daniel Arap Moi siku ya Jumatano.
- Ibada ya wafu ya kumuaga mzee Daniel Arap Moi inafanyika katika uwanja wa kitaifa wa michezo wa Nyayo na inatarajiwa kuanza saa nne asubuhi
- Mahema yanaendelea kuwekwa katika shule ya Kabarak huku shughuli zingine za matayarisho zikiendelea
- Mwili wa aliyekuwa rais unatarajiwa kuwasili katika uwanja huu Jumatano asubuhi ukitokea Nairobi
- Marais 18 kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya kumuaga rais mstaafu Daniel Arap Moi
- Waombolezaji 30,000 wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya kumuaga Daniel Toroitich Arap Moi
- Shughuli ya mazishi itasimamiwa na jeshi la taifa, na kuongozwa na kanisa la African Inland Church.
- Ni familia pekee watakaoruhisiwa kushuhudia mazishi huku raia wakiwa wamepata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa siku tatu.
- Serikali imetoa hakikisho kwamba maandalizi ya mazishi ya Daniel Arap Moi yanaendelea vyema
- Raia na wageni wengine watahudhuria ibada lakini hawataruhusiwa kwenye mazishi yenyewe.
Tags
habari









