hekole Menberu, mwenye umri wa miaka 27,alikuwa na matumaini makubwa ya kupata ajira mara baada ya kumaliza shahada yake ya uhandisi wa kemikali(chemical engineering) miaka miwili iliyopita nchini Ethiopia.
Ulikuwa ni wakati wa ukombozi, akiangalia miaka aliyoteseka kufikia kiwango hicho cha elimu cha chuo kikuu.
Kwa miaka mingi amekuwa akisafisha viatu barabarani ili aweze kujikimu kimaisha.
Tangu akiwa mdogo, bwana Chekole alikuwa anafanya shughuli za mtaani.
Baba yake alifariki wakati yuko mdogo hivyo akahamia wa babu na bibi yake waliopo Fogera katika eneo la Amhara. Sehemu ambayo mama yake aliolewa tena.
'Nilikuwa ninasumbua kutaka kwenda shule'
Alitaka sana kwenda shule lakini babu na bibi yake hawakuwa na uwezo wa kumlipia ada na kumhudumia katika matumizi mengine.
Hivyo aliamua kwenda nyumbani kwa mjomba wake na kumsidia kazi za ufugaji.
Ila alikuwa ana matumaini kuwa babu na bibi yake wataweza kumsaidia.
"Nilikuwa ninawasumbua sana babu na bibi yangu wanipeleke shule," aliiambia BBC.
Baadae, walikubali maombi yake na kumtaka aende kujiandikisha katika shule ya umma iliyopo mjini Woreta.
Lakini msaada wa babu yake ulikatika ghafla alipokuwa darasa la pili.
"Ilinibidi niondoke na kwenda mtaani kutafuta namna ya kujisaidia mwenyewe," alisema.
Kwa msaada wa rafiki yake ambaye a likuwa anasafisha viatu, na yeye pia akaanza kazi hiyo.
Tangu akiwa darasa la tatu mpaka alipomaliza chuo kikuu, fedha ambayo alikuwa anaipata na kulipia ada ilitoka kwenye kazi yake ya kusafisha viatu.
"Nilidhani kuwa kusafisha viatu ni kazi ambayo ingeweza kunisaidia.Nusu siku nilitumia kufanya kazi na nusu siku nilitumia kusoma," alisema.
"Maisha yalikuwa magumu sana. Lakini nilikuwa ninajipa moyo kwa simulizi za watu ambao walikuwa wanafikiri kama mimi na mwisho wa siku wakawa madaktari au wahandisi."
'Nilikuwa nimekata tamaa'
Kila mwaka wa masomo ulipoanza msongo wa mawazo ndio ulipoanza kwa sababu ilimbidi kununua sare za shule ambazo alikuwa anapata wakati mgumu sana kuweza kumudu kuzinunua.
"Elimu ilinigharimu sana", alisema.
"Nilikutana na wakati mgumu mara nyingi, lakini siwezi kusahau jinsi nilivyokuwa nakata tamaa, nilipokuwa kidato cha nane mpaka 10 na mwaka niliojiunga chuo kikuu."
Pamoja na changamoto nyingi ambazo alikutana nazo, mwaka 2013,ambapo alifanikiwa kuingia kuingia chuo kikuu cha Bahir Dar, katika mji mkuu wa Amhara ambapo alisomea 'chemical engineering'.
"Kulikuwa na uvumi kuwa nchi inahitaji wahandisi wengi katika viwanda ndio maana niliamua kusomea masomo ya uhandisi. Nilikuwa natumaini kuwa nitaajiriwa nikihitimu masomo yangu," alisema.
Maisha yake ya chuo kwa miaka mitano yalikuwa magumu kama ilivyokuwa awali.
Pamoja na barua kutoka wakiwa wanataka msaada kutoka kwangu, wakati huo chuo kilikuwa kilikuwa kinanilipa dola 10 kwa mwezi.
"Nilikuwa nikipata msaada kutoka kwa marafiki zangu na wanafunzi niliokuwa nakaa nao. Lakini wakati siku ya kuhitimu chuo ilipokaribia, hofu ilizidinikifikiria kama nitaenda kuajiriwa baada ya kuhitimu chuo kikuu.
"Nilikuwa na hofu kuwa sitapata ajira,"alisema.
'Sikuwa na bahati'
Mwaka 2017, bwana Chekole alihitimu shahada ya uhandisi na jambo la kwanza alilolifanya ni kutafuta ajira.
Lakini hakuweza kufanikiwa.
"Nilitumia miezi mitatu kutafuta ajira katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Nilizunguka katika viwanda vingi kutoka mji mmoja kuelekea mwingine ili kutafuta ajira lakini sikuweza kufanikiwa."
Alisafiri miji mingi bila mafanikio yoyote.
"Niliomba kaziambazo walikuwa hawataki kiwango cha shahada.Lakini maombi yangu yalikataliwa na waajiri wote.
Nilianza kazi kiwandani ambapi walikuwa wananilipa dola moja kwa siku lakini niliiacha kwa sababu kiwango kilikuwa kidogo kuweza kujikimu.
Ethiopia imekuwa ikiabiliana na changamoto ya kiuchumi hivi karibuni, vijana wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 29 katika maeneo ya mjini hawana ajira kwa mwaka 2018 iliyoongezeka kwa asilimia 22 kutoka mwaka 2016, kwa mujibu wa takwimu za nchi.
Wakati yupo chuo
Baada ya miezi adhaa ya kutafuta ajira ya elimu yake, alirudi Bahir Dar - na kufanya kazi ambayo akutegemea kurudi kufanya kazi ya aina hiyo.
"Nilipoona kuwa nilikuwa sina namna nyingine ya maisha, niliamua kwenda kufanya kazi ya kusafisha viatu tena."
Anasema kuwa anajilaumu kwenda shule, a nasema kuwa asingekuwa katika hali ngumu ya kiasi hiki kama angekuwa hajasoma.
"Elimu imenigharimu mno na sijapata tuzo katika changamoto zote alizopitia," alisema. "Nisingejitolea kiasi hicho kwa ajili ya kupata elimu"
Bwana Chekole alilalamikia serikali ya Ethiopia kwa kuangazia masuala ya siasa na usalama zaidi ya kutengeneza ajira kwa watu ambao hawana ajira.
"Walimu wangu walifahamu kuwa nilikuwa nnajilipia chuo kwa fedha nilizopata kwa kusafisha viatu, walinipa moyo na hata walikuwa wananisaidia na ela."
"Marafiki zangu niliosoma nao chuo walikuwa wanakuja kusafisha viatu vyao na kunipatia fedha."
Licha ya changamoto bado ana matumaini ya kupata ajira bado," alisema.