Serikali ya Marekani imetangaza kuwa, iko tayari kufanya mazungumzo na Iran bila masharti yoyote.
Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Kelly Craft ametangaza katika umoja huo kwamba, nchi yake ipo tayari kuanza mazungumzo na Iran bila masharti yoyote.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Rais wa Marekani Donald akizungumza jana katika hotuba yake kuhusiana na mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya kambi za kijeshi za nchi hiyo nchini Iraq alidai kuwa, hakuna raia wa Iraq au Marekani aliyeuawa katika shambulio hilo japo kambi hizo ziliharibiwa kidogo.
Trump alidai kwamba, Iran inaonekana kurudi nyuma, hatua ambayo ni nzuri kwa pande zote husika. Hata hivyo alisema kuwa, ataongeza vikwazo dhidi ya Iran.
Wakati Rais Trump akidai kwamba, hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa au kuuawa katika shambulio hilo, vyombo vya Iran jana vilisema kuwa Wanajeshi 80 wa Marekani waliuawa japo havikutoa uthibitisho wowote
Post a Comment
0Comments
3/related/default