Header Ads Widget

TETESI ZA SOKA LEO IJUMAA


 Manchester United wako tayari kusikiliza ofa kwa kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 31, mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, 30, na winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, huku meneja Erik ten Hag akijaribu kupunguza kikosi chake. (Independent)

Beki wa kati wa Everton Jarrad Branthwaite, 21, na mlinzi wa Crystal Palace Marc Guehi, 23, wako kwenye orodha ya watu wanaosakwa na Ange Postecoglou huku mkufunzi huyo wa Tottenham akiunda upya kikosi cha klabu hiyo. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Everton Dele Alli, 27, anakaribia kurejea kwenye mazoezi kamili huku akiongeza ahueni ya jeraha la paja ambalo limemaanisha kuwa bado hajacheza msimu huu. (Times – Subcription Required)

Fulham watamlenga kiungo wa kati wa Brazil Andre, 22, kutoka klabu ya Fluminense iwapo iwapo kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28, ataondoka Craven Cottage mwezi Januari. (Telegraph – Subscription Required)

Post a Comment

0 Comments