Wakati Albert Gilmour alipoitisha cheti za kuzaliwa kwake ili aweze kuoa, mamake alisita kumpatia.
Alipokipata cheti hicho mikononi mwake, kiliifichua siri ya familia.Mnamo 1965, akiwa na miaka 21 wakai huo, albert aligundua dadake mkubwa ni mamake mzazi.
"Ilikuwa ni hisia ya tamu uchungu," anakumbuka.
Alishtuka kugundua kwamba alilelewa na babu na bibi yake, Albert alimuuliza Ruby Gilmour maswali - "dadake" ambaye kwa hakika alikuwa ni mamake mzazi.


Aliuliza kuhusu babake, ambaye jina lake halikuwepo kwenye cheti hicho, na hakuamini alichoambiwa.
Albert alipewa jina la babake, Albert Carlow, kutoka Calais, Maine - ambaye alikuwa mojawapo ya wanajeshi waliokita kambi Ireland ya kaskazini wakati wa vita vya pili vya dunia.
Ruby alikuwa na miaka 17 alipokutana na mwanajehsi huyo shababu alipokuwa katika kambi liyo karibu na nyumbani kwa kina Ruby, Eglinton, County Londonderry.

Wazazi wake Albert walitengana mnamo 1944 msimu wa machipuko wakati babake alipotumwa kwa siri katika fukwa za bahari za Normandy.
Wakati Ruby alipojifungua mwezi Novemba, alimuita mwanawe jina la babake mtoto huyo aliyeamini alikuwa ameuawa vitani.
Kufuatia ufichuzi huo, Albert anasema aliamua kuyaacha kutokana na heshima kwa babu na bibi yake pamoja na mamake.
Lakini takriban miaka 35 baadaye, bintiye Albert Karen Cooke aliamua kufanya utafiti kuhusu familia ya babake kwa siri.
'Habari mbaya'
Alifanikiwa kumpata mojawapo wa mashangazi wake Albert kupitia anuani aliopewana bibi yake Ruby ambayo aliishika kichwani miaka 50 iliyopita.
Albert Carlow alimuandikia mepzni wake anuani hiyo nyuma ya pkiti ya sigara wakati wa vita.
"zawadi nzuri ambayo ningepatia babangu ni kumkutanisha na familia yake," Karen anasema. "Ni sehemu yake ambayo daima nilijuwa imo moyoni mwake, Umarekani."
Katika mawasiliano ya usiku sana kwa shangazi yake, alipata habara mbaya kwamba babake alifariki miaka 20 iliyopita.
Lakini Albert alifurahi kusikia kwamba bibi yake mzaa baba bado angali hai na kwamba alikuwa na kaka wawili wa kambo.
Shangazi yake Albert alimpatia picha ya marehemu babake.
Kama picha inavyoonesha , hakuamini ufanano aliokuwa nao na babake.

"Walisema: ' Tunajua tunapokutazama wewe ni nani, tabia zako, utu wako wewe ni babako mtupu.'
Albert na Karen walisafiri kwenda Marekani kukutana na familia yake ambayo alisema ni kama "ndoto iliojiri kuwa kweli".
"Walisema: ' Tunajua tunapokutazama wewe ni nani, tabia zako, utu wako wewe ni babako mtupu.'
"Sikuwa na haja ya kueleza chochote, sikuhitaji kuthibitisha chochote".
Kwa hisia kubwa Albert alikutana na bibi yake kabla ya kusafiri kwenda kuona kaburi la babake.
"lilia kwa masikitiko, ilikuwa ni vigumu kwake," Albert anasema.
Albert alieleza kwamba babake hakurudi kwa mamake kama alivyoahidi kwasababu alitumwa kwenda Afrika kutoka Ufaransa kabla ya kusafirishwa kurudishwa moja kwa moja nyumbani mwishoni mwa vita hivyo.
Albert anasema alizungumza kwa mara nyingine tena na mamake siku chache kabla ya kufariki kuhusu haya.
- Manusura wa jumba la mateso: Ilikuwa 'kama moto wa jahanamu'
- Mpishi akamatwa kwa upishi wa bangi
- Maandamano Bukavu kushinikiza kusitishwa mgomo wa walimu
- Waasi Yemen wadai kuwakamata wanajeshi wa Saudia
"Nilimuambia: 'Huna sabau ya kuomba msamaha'."
Huku akitarajiwa kuingia miaka 75, Albert anasema anataka kuhadithia kuhusu maisha yake binafsi kwa mara ya kwanza.
Anaamini kuna watoto wengine wa wakati wa vita kama yeye "wasiojuwa pa kwenda au wanahisi aibu kulizungumzia".
Tags
MATUKIO