Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Tunduru, James Paulo (27), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua kwa kumpiga risasi mke wake.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho usiku wa kuamkia Oktoba 21, mwaka huu, baada ya kutokea ugomvi kati yao.
Kamanda
Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, amethibitisha kuwapo kwa tukio
hilo na kwamba chanzo cha kifo hicho ni ugomvi uliosababishwa na tukio
la wivu wa kimpenzi.
Kamanda alimtaja mtu aliyeuawa kuwa ni Beatha Kufuru (25), ambaye alikuwa muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru.
Kamanda
Marwa ambaye alikuwa akizungumzia tukio hilo akiwa njiani kwenda
Tunduru ili kujiridhisha na hali halisi, alisema mtuhumiwa huyo alimpiga
risasi tatu kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema
polisi wanaendelea na uchuguzi wa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.
Tags
habari