Mahakama ya Rufani Tanzania imetengua uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyobatilisha sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu.
Kutokana na hatua hiyo, kuanzia sasa Wakurugenzi wapo huru kusimamia uchaguzi.
Uamuzi
wa Mahakama ya Rufani, umetolewa na Msajili Elizabeth Mkwizu baada ya
Serikali kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu juu
ubatilisho wa sheria hiyo.
Katika uamuzi uliosomwa na Msajili wa Mahakama, Mkwizu amesema kuwa miongoni mwa hoja ni kwamba;
Wakurugenzi
hawawi wasimamizi wa Uchaguzi moja kwa moja kwa kuteuliwa kwao bali
kuna mchakato wa kisheria wanapitia ikiwemo kula kiapo, kutunza siri na
kukana uanachama wa Chama walichokuwa nacho kabla ya uteuzi.
Mei
13, 2019 Serikali ilitangaza kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mei 10,
2019 uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo ilibatilisha sheria
inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu.
Uamuzi
huo ulitolewa na Jaji Atuganile Ngwala katika kesi ya msingi namba 6 ya
mwaka 2018 iliyofunguliwa na mtoto wa marehemu Chacha Wangwe ambaye ni
Bob Chacha Wangwe.
Katika
kesi hiyo ya Kikatiba, Jaji Ngwala alibatilisha vifungu viwili vya
Katiba cha 7 (1) ambapo kinaeleza kuwa ‘Kila Mkurugenzi wa Jiji na
Halmashauri wanakuwa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu’
Pia
alibatilisha Kifungu cha 7 (3) kinachoeleza kuwa Tume inaweza kumchagua
mtu yoyote kuwa msimamizi wa Uchaguzi wakati katiba inasema huwezi kuwa
Mwanasiasa na ukawa msimamizi wa uchaguzi bali inatakiwa achaguliwe mtu
huru.