As Roma yawa timu ya kwanza ya Ulaya kufungua Twitter ya Kiswahili

Admin
By -
0


Timu ya soka ya 'As Roma' ya nchini Italia imekuwa klabu kubwa ya kwanza barani Ulaya kuanzisha ukurasa wake katika mtandao wa Twitter kwa lugha ya Kiswahili.


Ukurasa wa klabu hiyo mashuhuri nchini Italia na barani Ulaya ambayo ilianzishwa mwaka 1927 utakuwa ukiandika habari zake kwa lugha adhimu ya Kiswahili.

Ukurasa huo wa lugha ya Kiswahili ulizinduliwa rasmi jana, na inaaminika lengo kuu la 'As Roma' ni kuwafikia mamilion ya watu wanatumia lugha ya Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani.

Baada ya kuzinduliwa ukurasa huo, wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili katika maeneo mbalimbali wameonekana wakipongeza hatua hiyo na kuanza kutoa maoni yao katika ukurasa huo. 

Msimamizii wa ukurasa huo ameandika haya baada ya kuzinduliwa ukurasa huu: Ahsante kwa upendo na ushirikiano ambao mmetuonyesha tangu tumezindua ukurasa huu rasmi. Ni dhahir kwamba, kwa pamoja tutaendelea kushirikiana na kufurahia pamoja hapa hapa kwa lugha ya Kiswahili.
Itakumbukwa kuwa katika mkutano wake mwezi uliopita huko jijini Dar es Salaam Tanzania Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ilipitisha pendekezo kuwa Kiswahili kianze kutumika kama lugha ya nne katika jumuiya hiyo.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)