Marekani inatarajiwa kujitoa rasmi katika mkataba wa nyuklia na Urusi, hatua inayozusha hofu kuhusu ushindani wa silaha mpya.
Mkataba huo unaohusu zana za nyuklia za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987.
Ulipiga marufuku makombora ya masafa ya kati ya kilomita 500-5,500.
Lakini awali mwaka huu Marekani na Nato ziliishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa kufyetua aina mpya ya kombora, jambo ambalo Moscow inalikana.
Marekani imesema ina ushahidi kuwa Urusi imetuma kombora aina ya 9M729 linalofahamika kwa Nato kama SSC-8. Tuhuma hizi ziliwasilishwa kwa washirika wa Nato wa Marekani ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani.
Rais Donald Trump mnamo Februari ametangaza kuwa Marekani itajitoa kutoka mkataba huo iwapo Urusi haitotii, na kuweka tarehe ya mwisho kuwa Agosti 2.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesitisha majukumu ya taifa lake katika mkataba huo muda mfupi baadaye.
Kuna hatari gani?
"Breki ya thamani katika vita vya nyuklia" inaeleka kupotea, ameonya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres.
"Huenda hili likaongeza na sio kupungua tishio la makombora," aliongeza, na kuomba pande zote kutafuta "makubaliano mapya ya mtazamao wa pamoja ya udhibiti wa silaha kimatiafa".
Wachambuzi wanahofia kwamba kutibuka kwa makubaliano hayo ya kihistoria huenda kukachangia ushindani mpya wa silaha kati ya Marekani, Urusi na China.
"Kutokana na kuvunjika kwa mkataba huo sasa, tutashuhudia utengenezaji na utumiaji wa silaha mpya," Pavel Felgenhauer, mchambuzi wa zana za Urusi ameliambia shirika la habari la AFP. "Urusi tayari ipo tayari."
Mwezi uliopita, Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg ameiambia BBC kuwa makombora ya Urusi - ambayo alisema kuwa ni "ukiukaji wa wazi wa mkataba huo" - zina uwezo wa nyuklia, ambayo ni magumu kutamabua na yanaweza kufika katika miji ya Ulaya katika muda wa dakika.
"Hili ni jambo zito," aliongeza. " Mkataba wa INF umekuwa jiwe la msingi katika udhibiti wa silaha kwa miongo kadhaa, na sasa tunashuhudia kuvunjika kwa mkataba huo ."
Ameongeza kwamba hakujakuwepo "ishara zozote" kuwa Urusi itatii na makubaliano hayo na kwamba "ni lazima tujitayarishe kwa ulimwengu usiokuwa na mkataba wa INF na ulio na makombora zaidi ya Urusi".
Stoltenberg pia alisema kuwa uamuzi wowote wa Nato kuhusu namna gani ya kujibu utatolewa baada ya kupita muda huo wa mwisho uliotolewa.
nato haina mpango wa kutuma makombora yake ya ardhini Ulaya lakini makombora ya angani na ya ulinzi, ya mazoezi na utayari wa vikosi vyake na mipango mipya ya udhibiti wa silaha huenda yakawa ni sehemu ya jibu lake.
Mkataba wa (INF) ni nini?
- Ulisainiwa na Marekani na uliokuwa Muungano wa Sovieti mnami 1987, mkataba huo ulipiga marufuku silaha zote za nyuklia na makombora yasio ya nyuklia ya masefu marefu na ya wastani isipokuwa ya baharini.
- Marekani ilikuwa na wasiwasi kuhusu kutumwa kwa kombora la SS-20 la Sovieti mnamo 1979 na ilijibu kwa kuweka makombora ya masafa mafupi ya ardhini Ulaya - hatua iliyozusha maandamano makubwa.
- Kufikia 1991, takriban makombora 2,700 yaliharibiwa.
- Mataifa hayo mawili yaliruhusiwa kukagua hifadhi za taifa mwenza.
Mambo yaliharibika wapi?
Mnamo 2007, rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza kuwa mkataba huo haushughulikii maslahi ya Urusi.
Hilo lilifanyika baada ya rais wa Marekani George W Bush, mnamo 2002, kuitoa Marekani katika mkataba wa kupinga makombora ya masafa ya juu, uliopiga marufuku silaha zilizoundwa kuzuia makombora ya aina hiyo.
Mnamo 2014, rais wa wakati huo Marekani Barack Obama aliishtumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo wa INF baada ya kutuhumiwa kufanya majaribio ya kombora la ardhini.
Inaarifiwa aliamua kutojitoa katika mkataba huo chni ya shinikizo la viongozi wa mataifa ya Ulaya, waliosema hatua kama hiyo huenda ikachangia ushindain wa umiliki wa silaha.
Alafu mwaka jana, Nato ikaunga mkono tuhuma za Marekani na kuishutumu rasmi Urusi kwa kukiuka mkataba huo.
"Washirika wamehitimisha kuwa Urusi imeunda na kutumia kombora 9M729, hatua inayokiuka mkataba wa INF na kuzusha hatari kwa usalama kati ya Ulaya na Atlatiki," taarifa kutoka mawaziri wa mambo ya nje wa Nato imeeleza.
taarifa hiyo imesema mataifa wanachama "yanaunga mkono" tuhuma za Marekani kuwa Urusi inakiuka mkataba huo, na kuoa wito kwa Moscow "irudi kutii kwa dharura na kikamilifu mkataba huo".
Urusi imekana tuhuma hiyo na rais Putin amesema ni kisingizio kwa Marekani kujito akatika mkataba huo.
Huku uhusiano kati ya Washinto na Moscow ukizidi kudorora, Uturuki mwezi uliopita ulipokea sehemu ya kwanza ya mfumo wa kombora la ulinzi S-400 licha ya upinzani kutoka Marekani.
Marekani imeonya kuwa Uturuki haiwezi kumiliki kwa pamoja mfumo huo wa S-400 na ndege za kivita za Marekani aina ya F-35.
Uturuki na Marekani sio washirika wa Nato lakini Uturuki imekuwa ikiidhnisha ushirikiano wa karibu na Urusi.