Anselem Sanyatwe: Marekani yamuekea vikwazo mjumbe wa Zimbabwe Tanzania

Admin
By -
0
Anselem Sanyatwe
Zimbabawe imeleza kutofurahishwa pakubwa kwa hatua ya Marekani kumuekea vikwazo Anselem Nhamo Sanyatwe, balozi wake nchini Tanzania.
Katika taarifa ya hivi punde, serikali ya Harare hiyo imeitaja hatua hiyo ya Marekani kama inayodunisha uhuru wa taifa hilo na ambayo 'inashinikiza migawanyiko badala ya kuidhinisha uponyaji wa taifa na maelewano'.
Wizara ya mambo ya nje Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya Balozi Sanyatwe, ambaye ni Brigedia mstaafu ya jeshi la kitaifa la ulinzi wa rais, kutokana na "kuhusika kwake katika ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu."
Wizara hiyo Marekani imefafanua kuwa ina taarifa za kuaminika kwamba Anselem Sanyatwe alihusika katika msako mkali dhidi ya raia Zimbabwe ambao walikuwa hawakujihami wakati wa ghasia zilizozuka mnamo Agosti mosi mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu, uliosababisha vifo vya raia wasita.
Zimbabwe imesema inapokea kwa uzito hatua ya 'baadhi ya mataifa yenye nguvu' yaliojichukulia hatua binfasi kuidhinisha hatua ambayo 'ni wazi zipo nje ya mtazamo na barua ya tume iliyoidhinishwa Zimbabwe kuchunguza ghasia hizo za baada ya uchaguzi.
Harare imeendelea kusema katika taarifa yake rasmi leo kuwa vikwazo hivyo ni kinyume cha sheria na 'kushinikizwa kwa hatua nyingine kama hiyo itakuwa haina manufaa.
Sanyatwe ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha jeshi la ulinzi wa rais, na sasa ni balozi wa Zimbabawe Tanzania aliushutumu upinzani kwa mauaji hayo katika ushahidi aliotoa mbele ya tume hiyo ya uchunguzi ilioyongozwana rais mstaafu wa Afrika kusini Kgalema Motlanthe.

Ghasia kati ya upinzani na maafisa wa usalama

Mnamo Agosti mosi mwaka jana ghasia zilizuka nchini Zimbabwe kati ya wafuasi wa upinzani na vikosi vya usalama katika mji mkuu wa Zimbabwe huku kukiwa na maandamano dhidi ya kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Magari yaliobeba maji ya kuwatawanya waandamanaji na vitoa machozi yalitumiwa katika barabara muhimu za mji wa Harare baada ya wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC Alliance kuweka vizuizi katikati ya mji huo.
Watu sita waliuawa katika maandamano hayo ya wafuasi wa chama cha upizani cha MDC mjini Harare yaliobadilika na kuwa mabaya nyakati za mchana.
Vikosi vya usalama vikikabiliana na waandamanaji Haki miliki ya picha Reuters
Makundi ya waandamanaji yalikuwa katikati ya mji huo tangu alfajiri lakini habari zilipozuka kwamba Zanu Pf kimeshinda viti vingi katika bunge na kwamba matokeo ya urais hayakuwa tayari, hali ilibadilika.
Walifanya maandamano katika barabara muhimu mjini Harare na kuelekea katika ofisi za zamani za chama cha Zanu Pf wakibeba mawe makubwa, fimbo na chochote kila ambacho wangeweza kubeba.
Kundi hilo lilisema 'tunamtaka Chamisa', wanaamini kwamba uchaguzi huo umekumbwa na udanganyifu na sasa wanataka mgombea wa MDC kutangazwa mshindi.
Matokeo yalionyesha kwamba Zanu-PF kilishinda viti vingi vya ubunge katika uchaguzi huo tangu kung'atuliwa madarakani kwa Robert Mugabe.
Chama cha upinzani cha muungano wa MDC kilisema kwamba kura hiyo ilifanyiwa udanganyifu na kwamba mgombea wake Nelson Chamisa alikuwa ameibuka mshindi.























































































































































































































































































































































































Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)