
Idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imeidhinbisha uuzaji wa silaha kwa Taiwan , utakaogharimu $2.2bn (£1.76bn), Pentagon imesema.
Mpango huo ni wa vifaru 108 , makombora 250 na vifaa vinavyohusiana.Mwezi uliopita , wixzara ya maswala ya kigeni nchini China iliitaka Marekani kusitisha uuzaji huo , ukiutaja kuwa swala nyeti na uamuzi mbaya.
China unaichukulia eneo la Taiwan kuwa miongoni mwa himaya yake ambayo inafaa kuunganishwa na nchi kavu kwa nguvu iwapo zitahitajika.
Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni geng Shuang pia aliitaka Marekani kuheshimu sera ya China ya taifa moja ambapo marekani inatambua China na sio Taiwan.
Uuzaji wa silaha hizo hautaathiri uwezo wowote wa kijeshi katika eneo hilo , ilisema marekani. Idara ya ulinzi tayari imelieleza bunge kuhusu uuzaji huo wa silaha.

Afisi ya rais wa Taiwan imeelezea furaha yake kwa Marekani ambayo ndilo taifa linalouzia taiwan silaha.
Msemaji wa rais wa taiwan alisema katika taarifa kwa reuters kwamba kisiwa hicho kitendelea kuimarisha uhusiano wake ewa kiusalama na Marekani.
Jeshi la Marekani laanzisha doria Kusini mwa Bahari ya China

Meli ya Marekani ya kubeba ndege za kivita ya USS Carl Vinsion imeanza kile kinatajwa kuwa oparesheni za kawaida kusini mwa bahari ya China, ikiandamana na meli zingine za kivita.
Oparesheni hiyo inakuja siku chache baada ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya China kuionya Marekani kwa kupinga uhuru wa China katika eneo hilo.
China inadai kumiliki maeneo kadha ya eneo la bahari ya kusini mwa China.
Imekuwa ikijenga visiwa bandia vilivyo na viwanga vya ndege kwa miaka kadha.

Meli hiyo ya kubeba ndege za kijeshi ilipitia mara ya mwisho eneo la kusini mwa bahari ya China miaka miwili iliyopta, wakati wa mazoezi na jeshi la Malaysia, na imefanya safari 16 kwa miaka 35 ya huduma yake.
Muda mfupi baada ya Donald Trump kuchukua uongozi mwezi Januari, utawala wake uliapa kuizuia China kudhibiti eneo la Kusini mwa bahari ya China.
Siku ya Jumatano msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini China Geng Shuang, aliitaka Marekani kutochukua hatua ambayo itapingauhuru na usalama wa China.
Tags
Kimataifa