Kutoka nchini Kenya nakusogezea taarifa inayohusu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga kilichopo Bondo asubuhi ya leo February 10, 2018wameanzisha vurugu kufuatia kifo cha mwenzao aliyekuwa klabu ya usiku siku ya Ijumaa jioni.
Wakati wa maandamano na vurugu hizo, wanafunzi hao wamechoma moto klabu ya usiku, ambapo mwenzao huyo alichomwa kisu hadi kupoteza maisha na kufanya shughuli zote za eneo hilo ikiwa ni pamoja na shughuli za biashara katika eneo hilo la Bondo kusimama.
Kifo cha kijana huyo kilitokea baada ya ugomvi kutokea ukimuhusisha marehemu huyo na wenzie kuhusu mwanamke jambo lililofanya mabaunsa wa klabu hiyo kuingilia kati, hadi kijana huyo kuchomwa kisu. Alipelekwa hospitali lakini alipoteza maisha pindi tu alipofika.
TAZAMA HAPA UTANI WA MAU FUNDI KWA TIMU YA YANGA...pia usisahau KUSUBSCRIBE

Tags
Kimataifa