ALICHO JIBU OKWI BAADA YA KUTO ONEKANA UWANJANI MUDA MREFU

Emanuel Okwi hakuonekana uwanjani kwa mechi kadhaa za ligi kuu lakini pia hakuwa sehemu ya kikosi cha simba kilichoshiriki mapinduzi Cup Zanzibar na kutolewa katika hatua ya makundi. Amerejea siku chache kabla ya mchezo wa simba dhidi ya Singida United.

Kutokuwepo kwa Okwi ndani ya kikosi cha Simba kulisababishwa mambo mengi kuzungumzwa, lakini katika mchezo huo dhidi ya Singida United aliingia dakika ya 66 kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin. Okwi aliifungia simba mabao mawili na kuisadia kuibuka na ushindi wa magoli 4-0

“Klabu ilikuwa inajua kitu gani kilitokea, enka zangu zilikuwa na maumivu fulani lakini sasa hivi nimerudi nawashukuru wachezaji wenzangu kwa kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kufanikiwa kupata haya magoli nawashukuru pia  mashabiki wamenipokea vizuri, tumerudi kuja kupambana tena”-Okwi.


Post a Comment

Previous Post Next Post