SPIKA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ASHINDWA KUPATIKANA BAADA YA MVUTANO MKALI KUIBUKA


Makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha, Tanzania.
Jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)  lililokoa Arusha Tanzania

Hali ya mvutano imeibuka kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA)  kuhusu namna ya Kumpata Spika Mpya wa Bunge hilo.

Mvutano huo mkubwa uliibuka Jumatatu mjini Arusha, Tanzania, kuhusu ni wajumbe wa nchi zipi waliofaa kusimama ili kuchaguliwa kama spika wa bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mgogoro huo ulizuka pale Tanzania, Burundi na Rwanda ziliposimamisha wajumbe wao huku nchi zingine wanachama wa jumuiya hiyo zikipinga hatua hiyo.
Baadhi ya wajumbe walisema kwamba baadhi ya nchi zilizotaka kusimamisha spika hazikuwa na nia njema kwa sababu wajumbe wao walikuwa wamehudumu kama spika katika mabunge ya zamani na hivyo basi ilikuwa ni zamu ya nchi zingine kuwasimamisha wajumbe wao.

Post a Comment

Previous Post Next Post