KOREA YA KASKAZINI YALAUMIWA KWA KUDUKUA NA KUWEKA VIRUSI VYA KOMPYUTA KWA MAKAMPUNI LAKI 3 DUNIANI

A programmer shows a sample of the WannaCry locked encryption page on a laptop
Kompyuta Zilizodukuliwa na kuwekea virusi vya wannaCry
Utawala nchini Marekani unasema kuwa Korea Kaskazini ilihusika moja kwa moja na kirusi cha wannaCry kilichoadhiri hospitali, biashara na mabenki kote duniani mapema mwaka huu.
Kirusi hicho kilidaiwa kuvamia zaidi ya kampuni 300,000 kwenye mataifa 150 na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola
Thomas Bossert ambaye ni msadizi wa Rais Donald Trump, aliyasema haya kupitia jarida la Wall Street Journal.
White House Homeland Security adviser Tom Bossert speaks to reporters about the global WannaCry "ransomware" cyber attack in May
Thimas Bossert, Msaidizi wa Rais Donald Trump
Hii ndiyo mara ya kwanza Marekani imeilaumu Korea Kaskazimni kwa kirusi hicho.
Bw. Bossert anayemshauri Trump katika masuala ya usalama wa ndani wa nchi alisema kuwa madai hayo ni kutokana na ushahidi uliopo.
Serikali ya Uingereza na kampuni ya kompiuta ya Microsof waliilaumu Korea Kaskazini kwa kirusi hicho.
Kim Jong-Un in an image released by North Korean news agency on December 12, speaking into microphone at a munitions conference
Kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong- Unn
Mwezi Mei kompiuta zinazotumia Windows zilivamiwa na kirusi hicho na kufungwa ambapo watumiaji walitakiwa kulipa ili kuweza kupata data zao.
Lakini Korea ya Kaskazini haijibu tuhuma hizo

Post a Comment

Previous Post Next Post