Nembo ya Mtandao maarufu wa Kijamii wa Facebook |
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo, Facebook ilikuwa ikikiuka sheria kwa kuyaunganisha mashirika mengine kwenye data za watumiaji wa mtandao huo.
Facebook ambayo inaimiliki pia mitandao ya Whatsapp na Instagram inabadilishana data za watumiaji katika mitandao hiyo na pia katika makampuni mengine, na hilo ni tatizo kubwa, limesema shirika hilo la nchini Ujerumani.
Shirika hilo limesema mienendo hiyo inakiuka sheria za Ulaya kuhusu haki ya faragha ya watumiaji.
Facebook inachunguzwa barani Ulaya kuhusiana na ubadilishanaji huo wa data za watumiaji, na inakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Ulaya kuhusiana na kuzitoa data binafsi za watumiaji wa Ulaya kwa Marekani
Tags
social media