SIMBA WATANGAZA KUMUHITAJI KOCHA HUYU

Kocha Kopunovic kushoto na Suleiman Matola Kulia..

Taarifa za uhakika ni kwamba uongozi wa Simba umefanya mazungumzo na kocha wake wa zamani Goran Kopunovic ili arithi mikoba ya Omog aliyetimuliwa jana.

Aidha wakati Simba ikimnyemelea kocha huyo, kuna taarifa iwapo kama dili la kumnasa Kopunovic litakwama, Simba inaweza kumrejesha nyumbani Selemani Matola, kocha wa Lipuli FC ili aje kuwa kocha msaidizi na Masudi Djuma kuwa kocha Mkuu.

Mbadala wa Omog anatarajiwa kutangazwa siku chache zijazo.

Kwa sasa timu iko chini ya kocha Msaidizi Masudi Djuma.


Post a Comment

Previous Post Next Post