SERIKALI KUAJIRI WALIMU WAPYA 11,000


Image result for picha za JAfo
Seleman Jafo, Waziri wa TAMISEM
DODOMA:
Serikali inatarajia kuajiri walimu wapya zaidi ya 11,000, wa shule za msingi na sekondari kwa mwa wa 2017/18.

Ahandi hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo  leo na Umoja wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) mjini  Dodoma wakati wa kurekodi kipindi cha Tujadiliane na kuongeza kuwa katika mpango huo walimu 7000 watakuwa wa shule za msingi na sekondari watakuwa 4,000.


Jafo amesema kuwa walimu hao watakaoajiriwa wataziba pengo la upungufu wa waliom uliotikana na kuonguezaka kwa idadi ya wanafunzi walioandkishwa toka sera ya elimu bure ianze kutumika.

Waziri huyo ameziomba taasisi na wadau wa elimu kuunga mkono sera ya elimu  buru ili kuisaidia serikali kufanikisha mpango huo.

"Natoa wito kwa taasisi na wadadu mbali mbali wa elimu tuungane sote ili kutekeleza hii sera na tufanikishe leongo letu". amesem Waziri Jafo.

 Kuhusu upungufu wa miundombinu Jafo amesema kuwa serikali imetenga bilioni 82 zitakazotumika kujenga vyumba vya madarasa, na matundu ya vyoo.

Post a Comment

Previous Post Next Post