Kocha wa Lipuli ya Iringa, Seleman Matola amesema anasubiri kwa hamu taarifa za Simba kuwa wanamhitaji zimfikie mezani, kwani tetesi anazosikia kwenye vyombo vya habari zimemchosha.
Matola ambaye anasaidiana na Amri Said kuinoa Lipuli, anadaiwa kutakiwa na Simba ili akamsaidie Mrundi Masoud Djuma ambaye sasa amekabidhiiwa mikoba ya kuifundisha timu hiyo baada ya Mcameroon Joseph Omog kutupiwa virago.
“Kila kukicha vyombo vya habari ni Matola kwenda Simba, lakini habari hizo hazijanifikia kabisa zaidi ya kusikia tu mimi nasubiri siku hiyo watakapofika mezani,” anasema Matola.
“Sina tatizo na Simba na mkataba wangu na Lipuli haunibani hata nishindwe kuondoka lakini mambo yote naweza kuyazungumza vizuri ni pale Simba watakapofika mezani.”
Awali, Matola alikuwa mchezaji wa zamani na nahodha tegemeo wa Simba, lakini baadaye akapewa nafasi ya kocha msaidizi aliwasaidia kwa vipindi tofauti, Golan Kuponovic na Dylan Kerr.

Tags
Michezo