TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa gari dogo aina ya Toyota Land Cruiser (Prado) linadaiwa kuseleleka kutoka kwenye pantoni (Ferry) na kuzama baharini eneo la Posta jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi, Desemba 1, 2017.
Inadaiwa kwamba katika gari hilo binafsi kulikuwa na watu wanne ambao wote walizama nalo na mpaka tunaenda mitamboni ilikuwa haijajulikana kama wamenusurika au wamekufa.
Video hiyo inaonesha watu wakishangaa eneo la tukio huku mmoja wao akijitolea kwenda kulifunga kamba gari hilo ili livutwe na kuokolewa lakini kabla ya kulifikia, lilizama baharini na kupotea.
Mtandao wa SWAHIBA BLOG umemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, kuzungumzia tukio hilo ambapo amesema hana taarifa kwa kuwa alikuwa kwenye kikao hivyo anakwenda kufuatilia na atatoa ufafanuzi kuhusu tukio iwapo limetokea.

Tags
MATUKIO