Luis Suarez alipatia Barcelona bao la kwanza mnamo dakika ya 54 naye Lionel Messi akapachika bao la pili kwa njia ya mkwaju wa penalti, baada ya Dani Carvajal wa Real madrid kuoneshwa kadi nyekundu kwa kuzuia mpira langoni akitumia mkono.
Bao la tatu lilitiwa kimiani na Aleix Vidal.
Ushindi huo unaiweka Barcelona pointi 14 mbele ya Real madrid.
Tags
Michezo