YANGA YAANZA KUMWAJIBISHA DONALD NGOMA

Yanga imeanza mchakato wa kusaka mbadala wa mshambuliaji raia wa Zimbabwe Donald Ngoma ambaye amekalia kuti kavu klabuni.

Tayari kamati ya usajili inayoongozwa na Mwenyekiti Hussein Nyika imeshusha washambuliaji watatu wa Kimataifa ambao watafanyiwa majaribio mmoja akitarajiwa kusajiliwa

Washambuliaji hao Bensua Da Silva kutoka Guinea Bissau, Badara Kerra kutoka Sierra Lione na Adam Zikiru kutoka Ghana wanamsubiri kocha Mkuu George Lwandamina anayetarajiwa kuwasili wikiendi hii akitokea mapumzikoni kwao nchini Zambia.

Aidha Donald Ngoma aliyewasili jijini Dar es salaam juzi tayari ameshaandikiwa barua ya kujieleza baada ya kuondoka kambini kwa zaidi ya wiki sita bila kuutaarifu uongozi.


Post a Comment

Previous Post Next Post