![]() |
| Kushoto ni watalii wa kimarekani na kulia ni Hekalu la Kibudda nchiniThailand (Picha ya Mtandao) |
Raia wawili wa Marekani wamekamatwa nchini Thailand baada ya kuchapisha picha yao mtandaoni wakionyesha makalio yao katika hekalu.
Watalii hao walipiga picha hiyo katika hekalu maarufu nchini Bangkok Wat Arun na kuichapisha katika mitandao ya Twitter na instagram.
Mamlaka ya uhamiaji ilisema kwamba kwamba wawili hao Joseph na Travis Dasilva wote wakiwa na umnri wa miaka 38 watapigwa faini na kurudishwa kwao.
Thailand ina sheria kali kuhusu tabia zinazoonekana kutokuwa na heshima na zinazoingilia dini yake ya Buddha.
![]() |
| Katika ni Watailii waliokamatwa wakiwa chini ya ulinzi na Jeshi la uhamiaji nchini Thailand(Picha ya Mtandao) |
Watalii hao walikamatwa jion wakati walipokuwa wakiondoka nchini humo katika uwanja wa ndege wa Bankok Don Mueang.
Naibu msemaji wa idara ya uhamiaji nchini Thailand, kanali Choengron Rimpadee aliambia BBC kwamba wawili hao walikuwa katika orodha ya watu waliokuwa wakichunguzwa baada ya mamlaka kuona picha hizo zenye utata katika mitandao ya kijamii.
''Wakati watakaposhtakiwa maafisa wa polisi wa uhamiaji wa Thailand watafutilia mbali visa zao na kutaka warudishwe makwao'', alisema.
Tags
VITUKO

