Tayari ndio tuko robo tu ya msimu wa ligi wa soka barani Ulaya 2017/2018 lakini tayari baadhi ya timu zimeshaanza kuona makucha, Lioneil Messi naye ameshaona timu ambazo msimu huu ni tishio kubwa.
Messi amesema msimu huu timu nyingi zinaonekana bora lakini kwa mtazamo wake zipo timu ambazo ukienda vibaya msimu huu zinaweza kukushushia dhahma kubwa ya mabao kutokana na ubora wake.
Katika timu ambazo Messi anazihofia namba moja ni timu ya kocha wake wa zamani Pep Gurdiola Manchester City ambao sio Ulaya sio Uingereza wanaonekana kutoa dozi nzito kotekote msimu huu.
Achilia mbali Manchester City lakini pia Lioneil Messi anaamini uwepo wa Mbappe na Neymar katika timu moja unazifanya timu nyingi ikiwemo yeye kuwahofia Paris Saint German,nao poa amewaita tishio.
Bayern Munich nao wapo katika orodha ya timu hatari za Neymar huku wapinzani wakubwa wa Barca klabu ya Real Madrid pia wapo. Messi hawazi sana kuhusu mapungufu ya Madrid na anaamini ukubwa na nguvu ya timu hiyo unawafanya kuwa hatari mara zote.
Klabu zote hizo nne zinaweza kukutana na Barcelona katika hatua ya mtoano ya Champions League huku Barca wenyewe wakionekana wamerejea kwenye makali yao lakini Messi hatamani kukutana na timu hizo.

Tags
Michezo